Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Mada na Matukio

Desemba, 2010

Wanachama wa Kamati ndogo ya Kompyuta ya JOCV inatengeneza vipeperushi vya kuelimisha watumiaji wa Kompyuta

Katika miaka ya hivi karibuni, intaneti imeenea kwa haraka pamoja na maendeleo ya simu za mikononi, na hivi sasa uhalifu wa kutumia mtandao unaibuka.

Ingawa intaneti ndiyo inayoweza kuchangia kwenye maendeleo ya uchumi, kuna matumizi mabaya ya intaneti yanayosababisha matatizo katika nchi nyingi.

Zaidi ya hayo, jumuia ya intaneti kwa upana na usiri wake inatambulika na kanuni ya uwajibikaji binafsi wa mtumiaji. Uchaguzi wa taarifa na mada yanabaki kuwa jukumu la mtumiaji mwenyewe.

Kanuni hii bado haijaeleweka kikamilifu na watumiaji wa intaneti nchini Tanzania.

Kwa hali hii, tumetengeneza vipeperushi vya aina mbili; "Ulinzi wa Taarifa" na "Maadili ya Intaneti", kwa madhumuni ya kuzuia uhalifu wa kutumia mtandao, na kwa maendeleo ya Intaneti.

Ingawa vipeperushi hivi viko katika karatasi moja, tunaamini kwamba maudhui yaliyomo yanaweza kuwasaidia watumiaji wa Kompyuta kujua "Ulinzi wa Taarifa" na "Maadili ya Intaneti" ni nini. Yanaeleza pia nini watumiaji wanatakiwa kufanya.

Intaneti ni chombo cha manufaa ya kiwango cha juu sana katika maisha yetu.

Natumaini kwamba utaitumia vizuri ukizingatia ulinzi na maadili ya Intaneti. Vipeperushi hivi vitakusaidia kama kumbukumbu nzuri.

(Bw. Taichi YAMADA, JOCV wa Teknolojia ya Kompyuta, Masasi)

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency