Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Mada na Matukio

28 Desemba, 2010

JICA imetoa msaada wa Pikipiki 10 kwa Mamlaka 5 za Serikali za Mitaa

Ofisi ya JICA nchini Tanzania inaisaidia Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika utekelezaji wa mradi wa O&OD (Kuimarisha Mipango Shirikishi na duru ya Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya Utawala Bora wa Serikali za Mitaa) kwa miaka minne (Oktoba 2009 hadi Aprili 2013). Mradi huu unahusisha Mamlaka 5 za Serikali za Mitaa za Mikoa ya Morogoro na Pwani, ambazo ni Halmashauri za Wilaya za Ulanga, Morogoro, Kilombero, Bagamoyo na Kisarawe.

Katika mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa mradi huu (2009), baadhi ya mafanikio makubwa yameonekana kama vile kuundwa kwa vikosi kazi katika mikoa miwili, kuandaliwa kwa mtaala wa mafunzo na mafunzo ya wawezeshaji wa kata (uanzishaji wa mfumo wa utendaji kazi wa mafunzo kwa wawezeshaji wa kata). Zaidi ya hayo, wajumbe wa kikosi kazi cha mkoa walipelekwa Japani kwa ajili ya mafunzo Shirikishi ya Maendeleo ya jamii ya maeneo yao. Aidha, zana za picha za kufundishia kwa ajili ya uwezeshaji jamii zimeandaliwa.

Katika mwaka wa pili wa utekelezaji wa mradi huu (2010), JICA imetoa pikipiki 10 (mbili kwa kila mamlaka ya mitaa) kwa ajili ya kutumiwa na Wawezeshaji wa Kata wakati wa shughuli zao za kila siku za kuisaidia jamii katika mchakato mzima wa duru ya maendeleo ya jamii. Usafiri limekuwa ni tatizo la muda mrefu miongoni mwa maofisa wa serikali wanaofanya kazi katika ngazi ya kata, likiathiri ufanisi wao katika utoaji huduma. Inatarajiwa kwamba jitihada hii itapunguza ukubwa wa tatizo. Msaada wa usafiri utasaidia kuunganisha jamii na mamlaka za mitaa wakati wa utekelezaji wa duru nzima ya maendeleo ya jamii na kusaidia shughuli za sekta nyingine hususan ufuatiliaji katika ngazi hii.

pichaPikipiki 10 zilikabidhiwa kwa ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa tarehe 28 Desemba, 2010.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency