Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Mada na Matukio

6 Januari, 2011

Walimu wa Kijapani wafika Tanzania kufanya kazi kwa miaka miwili

picha

Tarehe 6 Januari, 2011, vijana wa Kijapani 17 kutoka Japani walifika Tanzania na watafanya kazi na watu wa Tanzania katika sekta mbalimbali, hasa sekta ya elimu.

Kati ya vijana hao 17 wanaojitolea, 14 ni walimu wa sayansi na hisabati katika shule za msingi na sekondari, utengenezaji wa magari, matengenezo ya vifaa vya umeme na elektroni, teknolojia ya kompyuta na utalii katika taasisi za mafunzo ya ufundi stadi. Wengine watatu watafanya kazi katika fani ya tiba ya viungo katika hospitali, usanifu wa ujenzi kimandhari, na shughuli za vijana katika asasi za serikali.

Bi. Tamura, mmoja wa Wafanyakazi wa Kujitolea kutoka Japani (JOCV) aliyefika siku hiyo na ambaye atafundisha sayansi na hisabati katika Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Masasi, anasema: "Ingawa mazingira ya Masasi ni tofauti na yale ya Japani, nina furaha na ninatarajia kukabiliana nayo, kwa kuwa ninaamini kwamba nitajifunza zaidi kutokana na mazingira hayo."

Kijana mwingine wa shirika hilo, Bw. Furuike, ambaye atafundisha Utalii katika Chuo cha VETA Dodoma, anaamini kwamba sekta ya utalii ni muhimu sana kwa Tanzania, na anasema atatumia uzoefu wake kuchangia katika maendeleo ya utalii nchini. Kabla ya kuja Tanzania, alikuwa akifanya kazi kwenye hoteli ya kitalii huko Tokyo, Japani.

Kwa sasa, JICA Tanzania ina wafanyakazi 66 wa kujitolea kutoka Japani nchini Tanzania. Tangu kuanza kwa programu hii nchini Tanzania mwaka 1966, jumla ya Wajapani wa kujitolea 1345 wameshaletwa nchini.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency