Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Mada na Matukio

17 Januari, 2011

JICA na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) wanasaidia walimu wa ufundi Tanzania kuongeza ujuzi wao wa kufundisha.

picha

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) Dar es Salaam RVTSC na JICA waliandaa semina ya kusaidia walimu 21 katika fani ya uhandisi wa magari kutoka shule mbalimbali za ufundi na taasisi za elimu ya juu ikiwa ni pamoja na VETA, Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC), Vyuo vya Ufundi Stadi (CTC) na Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT).

Kamati ndogo ya wafanyakazi wa kujitole kutoka Japani ya Uhandisi wa Magari, ambayo inaongozwa na Bw. Ryuji Oshita, na waratibu wawili wa Klabu ya Walimu wa Kutengeneza Magari Tanzania (TAMTC), Bw. Deogratius Lufunga na Bw. Erick M. Mpokwa walitoa mihadhara katika semina kuanzia Jumatatu ya tarehe 17 Januari hadi Ijumaa ya tarehe 21 Januari 2011.

Wakati wa semina hiyo walimu wa ufundi stadi walijifunza jinsi ya kutoa mhadhara kwa kuzingatia andalio la mhadhara wakiwa na vitini na sampuli za zana ili kuongeza uelewa mzuri wa wanafunzi. Semina ilitoa nafasi kwa washiriki kupitia upya njia iliyozoeleka ya utoaji mihadhara. Mijadala hai iliyofanywa na washiriki kupitia upya vipindi, iliwahakikishia kuwa wanakuwa na fikra tunduizi kuhusu njia za kufundishia na ubora wa mihadhara mwishoni mwa semina. Mada za mihadhara hiyo zilijumuisha masomo ya "Elektronic Fuel Injection ((EFI)", "Air Induction", Sensor, "Fuel System", na "Wire Diagram."

JICA inaendelea kuimarisha ushirikiano na taasisi za mafunzo ya ufundi stadi, ikiwa ni pamoja na VETA na FDC, ili kuwasaidia wananchi wa Tanzania.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency