Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Mada na Matukio

20 Januari, 2011

Wanafamilia wa Kijapani wawatembelea Wajapani wanaojitolea nchini Tanzania

picha

Tarehe 20 Januari, 2011, wageni kumi kutoka Japani waliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam. Ni wanafamilia wa baadhi ya wafanyakazi wa kujitolea kutoka Japani (JOCV), na walikuja hapa kuwatembelea vijana wao ambao wanafanya kazi za kujitolea kwa kupitia JICA. Kipindi hiki, Wajapani wanaojitolea watano miongoni mwa 66 ambao wanafanya kazi nchini waliwapokea wanafamilia wao hapa nchini.

Walipokuwa nchini, wanafamilia wote hao walitembelea maeneo ya vijijini ambako vijana wao wa kiume na kike walikuwa wanafanya kazi.

Bi. Noriko Komatsu, anayefanya kazi kama Muuguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea tangu Julai, 2009, alimpokea mama yake Chizuko mwenye umri wa miaka 60, na mdogo wake wa kike. Alisema: "Nina furaha sana kuwa na mama yangu na dada yangu hapa! Nilikuwa na wasiwasi kwa sababu hawajawahi kusafiri nje ya Japani".

Wanafamilia yao walitembelea Nachingwea mkoani Lindi ambako Noriko anaishi. Alipotua kwenye uwanja wa ndege mama yake Noriko alisema "Tangu Noriko aondoke kuja huku mbali Afrika mwaka mmoja na nusu uliopita, hii ni mara yangu ya kwanza kumwona binti yangu, na ninafurahi sana kumwona akiwa katika hali nzuri ya afya. Nasikia kuwa mahali anakoishi hakuna maji ya bomba na hakuna umeme. Ninatarajia kutembelea huko."

Bw. Yoshisada Watanabe (62), baba yake Ayako anayefundisha masomo ya sayansi na hisabati katika shule ya Sekondari ya Nanguruwe mkoani Mtwara, alikuwa hapa nchini na mke wake, Yasue. Naye alisema hivi: "Ninafurahi kumwona mtoto wangu akiwa na afya nzuri na nimemwona kama amekua kiakili. Mji wa Dar es Salaam unanikumbusha mji wa Singapore nilioutembelea miaka 35 iliyopita, hivyo hauonekani wa kushangaza kwangu".

Kijana wa Bw. Shin-ichi Takahashi, Taichi, ni mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kilingi huko Siha mkoani Kilimanjaro. Baba yake alisema, "Ndoto yangu ya muda mrefu safari hii itatimia kwa kumtembelea kijana wangu nchini Tanzania. Ninapenda milima, na nimekuwa na ndoto ya kuuona Mlima Kilimanjaro kwa muda mrefu!"

Akishangazwa na hali ya hewa ya joto Dar es salaam kwa wakati huo, Bi Akiko Anazawa, ambaye ni mama yake Tomoyo anayefanya kazi Mafinga, alisema "Tunatoka katika eneo lenye sm 30 za ulalo wa barafu. Sasa tumejikita hapa katikati ya majira ya joto".

picha

Bw. Masayoshi Ozaki, mdogo wake wa kiume wa Hisaaki anayefundisha utengenezaji wa magari huko Masasi, alisema kwamba teknolojia mpya ya mawasiliano inawafanya wahisi wako karibu. Anatambua kuwa uhusiano wao sasa ni madhubuti kuliko ulivyokuwa wakati kaka yake alipokuwa Japani. Ni kwa sababu wanawasiliana mara kwa mara kwenye intaneti.

Licha ya kutembelea asasi zilizowapokea vijana wao wa kike na kiume, wanafamilia hao pia walitembelea maeneo ya utalii ya Tanzania kama vile Zanzibar na Kilimanjaro katika wiki moja waliyokuwepo nchini.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency