Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Mada na Matukio

16 Febrari, 2011

Ziara ya Vyombo vya Habari huko Mbeya:Mradi wa Kuimarisha Uwezo kwenye Teknolojia Inayotumia Nguvu Kazi katika Chuo cha Mafunzo ya Teknolojia ya Nguvu Kazi (14-16 Febrari, 2011)

pichaWakazi wa Ilolo waliofanya kazi za ujenzi wa barabara wakizungumza kuhusu faida zitokanazo na barabara bora.

Wakisindikizwa na maofisa wa JICA Tanzania, kundi la waandishi wa habari nchini lilifanya ziara ya kuangalia shughuli za ushirikiano wa kiufundi wa Wajapani kuhusu teknolojia inayotumia nguvu kazi (LBT) katika Chuo cha Mafunzo ya Teknolojia ya nguvu kazi (ATTI) katika mkoa wa Mbeya, Kusini Magharibi mwa Tanzania.

ATTI, ambayo ni wakala wa Serikali, ilianza shughuli zake mwaka 1993 kwa madhumuni ya kuboresha LBT. Mwaka 2006, JICA ilianza kuisaidia chuo hicho kwa kuimarisha uwezo na uendelezaji wa mafunzo ya rasilimali watu kupitia vikundi mbalimbasli kama vile makandarasi, washauri/waelekezi, vikundi vya jamii, wahandisi na mafundisanifu.

Ili kutumia elimu iliyofundishwa katika chuo, ATT iliendesha majaribio ya mradi wa ujenzi wa barabara huko wilayani Mbozi na Rungwe, kwa kutumia mtazamo wa LBT. Mtazamo huu ulitumiwa katika ujenzi wa barabara za Ilolo-lyula, Ibungu na Ipagika ambazo zilikuwa hazipitiki hasa wakati wa msimu wa mvua. Hata hivyo, baada ya ujenzi wa barabara hizo, wakazi wa maeneo hayo walithibitisha, kupitia mahojiano, kwamba barabara sasa zinapitika na sasa wanaweza kusafirisha bidhaa zao za kilimo kwenda kwenye masoko, na pia watu wanahamasika kuwekeza kandokando ya barabara.

pichaBarabara ya Ibungu iliyojengwa na wanakijiji kwa kujitolea.

pichaKituo cha kukusanyia majani ya chai kando kando ya barabara ya Obungu. Wakulima wadogo huleta mazao yao hapa, na kampuni ya chai huja kuyachukua kwa gari.


Pamoja na matokeo haya, wakazi wa maeneo husika walisema kwamba LBT imewapa wananchi kazi na ujuzi katika maeneo ambayo miradi ilitekelezwa na pia huduma za jamii ziliboreshwa. Aidha, kwa kuzingatia hali ngumu ya uchumi iliyopo nchini, imedhihirika kwamba mtazamo wa LBT umeonekana kuwa njia inayofaa ya kujenga barabara nzuri, za bei nafuu na zinazodumu katika maeneo ya vijijini.

Baada ya ziara yao, kikundi cha waandishi wa habari kilichapisha makala katika magazeti na kutangaza katika kituo cha televisheni. Kupitia makala hizo wananchi walio wengi walizielewa zaidi shughuli za ushirikiano za JICA katika kukuza Teknolojia inayozingatia nguvu kazi nchini.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency