Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Mada na Matukio

Machi, 2011

Elimu ya watoto wadogo katika Mbeya

picha

Mimi ni mmojawapo wa wafanyakazi wa kujitolea kutoka Japani kupitia shirika la JICA, na nafanya kazi katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwenye sekta ya elimu ya watoto wadogo.

Kitu cha kwanza kilichonishangaza mara baada ya kufika Tanzania kilikuwa ni kuona takataka zilizosambaa barabarani na watu kuonekana kutojali hali hii. Zaidi ya hayo, niliona kwamba watu hawana tabia ya kutumia mapipa ya kuwekea takataka, na pia hutupa ovyo takataka barabarani. Kutokana na kuguswa na hali hiyo, niliamua kujihusisha na swali hili.

Kazi yangu kubwa ni kuangalia shule ya chekechea ambayo iko ndani ya halmashauri yetu. Pia natembelea mara kwa mara shule nyingine za watoto wadogo, chekechea, na nyumba za yatima katika maeneo ya jiji. Katika matembezi haya, nawafundisha misingi ya afya bora kama vile umuhimu wa kunawa mikono, kupiga mswaki, kutoa kamasi kutumia kitambaa, jinsi ya kutupa takataka na kadhalika. Kwenye mafunzo haya, natumia vifaa vya kufundishia kama wanasesere na michoro nilizotengeneza.

pichaMafunzo ya misingi ya afya bora (walimu wakiwafundisha watoto)

Nilianza kazi huku nikielewa wazi kwamba udadisi, moyo mpana na kasi ya kujifunza ya watoto inafanana katika dunia nzima. Utotoni ni wakati muhimu sana kwa ajili ya kujifunza swala la afya. Wakishajifunza msingi wa swala la afya utotoni, watoto watakua kufuatia na msingi huu.

Katika shule ya chekecheka na nyumba ya yatima ambayo ninatembelea mara kwa mara, JICA ilitoa msaada wa kutengeneza sehemu za michanga ya kuchezea. Kwa kutumia michanga, watoto huaanzisha michezo yenye ubunifu mkubwa. Katika sehemu hizi za michanga, watoto wanafurahia kutengeneza keki, milima na nyumba za mifano kwa kutumia bakuli au vifuu vya nazi. Ninataka watoto wajifunze na wapate hisia kubwa za ubunifu na uasili kupitia mchezo wa michanga katika nchi hii ambapo vifaa vya kufundisha ni haba.

Pia natembelea wodi ya watoto katika hospitali ya taifa na kuwasomea vitabu vya watoto. Ziara hii inasubiriwa sana na watoto wanaochoka kukaa vitandani kila siku, vilevile na wazazi wanaochoka na kazi za uuguzi.

pichaWatoto wakichaza katika sehemu ya michanga

Nilipofika nchini kwa mara ya kwanza, watoto wa Tanzania walikuwa wananiangalia kwa mshangao. Waliniita mtu wasiyemjua, kwa sababu nilitoka mbali. Lakini leo, baada ya mwaka mmoja na nusu, wakati wowote wakiniona, wananiita "mwalimu! mwalimu!" na wananikimbilia na kila mtoto anataka kuniongelesha. Huu ni wakati wa furaha sana kwangu kama ni mwana elimu wa watoto wadogo, na furaha ya watoto inanipa moyo wa kufanya kazi zaidi na zaidi.

Katika muda uliobaki, nitaendelea kufanya kazi nikiwa na watoto hawa wa Tanzania. Sitosahau jinsi watoto hawa walivyoweza kujenga maisha yangu na yao pia.

(Bi. Norie Sasaki, JOCV, Elimu ya Watoto Wadogo, Mbeya)

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency