Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Mada na Matukio

22 Juni, 2011

Wafanyakazi wa Kujitolea kutoka Japani wamemaliza muhula wao wa kazi nchini kwa ufanisi

picha

Wafanyakazi wa kujitolea kutoka Japani (Japanese Overseas Cooperation Volunteers) kupitia shirika la JICA ambao wamemaliza muda wao wa kufanya kazi waliondoka nchini tarehe 22 Juni, 2011. Kabla ya kuondoka nchini, wafanyakazi hawa watano walitembelea Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (UTUMISHI), tarehe 16 Juni, 2011.

Wataalamu hao watano walifanya kazi kwa muda wa miaka miwili katika sehemu mbalimbali kama ifuatavyo;

- Bi. Sayaka HOSOYAMADA: Elimu ya Sayansi na Hisabati: Shule ya Sekondari ya Ngudu, Mwanza
- Bi. Yumi KOYAMA: Elimu ya Mazingira: Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Mtwara
- Bi. Noriko KOMATSU: Uuguzi: Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea, Lindi
- Bi. Norie SASAKI: Elimu ya Watoto Wadogo: Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Mbeya
- Bw. Hayato WATANABE: Ufundi Magari: Chuo cha Ufundi Songea (VETA), Ruvuma

Katika ofisi ya UTUMISHI, kila mfanyakazi alitoa ripoti fupi juu ya kazi zake, na Bw. Gerge Yambeshi, Katibu Mkuu wa UTUMISHI, aliwasikiliza na kuwashukuru kwa michango yao katika muda wao wa kufanya kazi. Waandishi wa habari wa Tanzania pia walikuwepo na walitoa ripoti juu ya kazi zao katika vyombo vya habari mbalimbali.

Habari zaidi juu ya Wafanyakazi hawa;

Bi. Sayaka HOSOYAMADA alikuwa mwalimu wa hisabati katika Shule ya Sekondari ya Ngudu, Mwanza. Alifundisha hisabati kwenye O-level na A-level akilenga kuboresha utendaji wa wanafunzi na kuinua ari yao ya kusoma. Kwa kweli, wastani wa ufaulu katika mitihani ya shuleni hapo uliongezeka kutoka 9 mpaka 50 katika hiyo miaka miwili. Pia alijihusisha na kazi za utawala wa shule na kuwasaidia walimu wengine shuleni.

Ms. Yumi KOYAMA alifanya kazi kwenye elimu ya mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Mtwara. Aliendesha programu ya madarasa ya somo la mazingira kwenye shule za msingi, akiwa na kauli mbiu hii; "Kutunza mazingira yetu ni sawa na kutunza maisha yetu". Katika programu hii, aliwafundisha wanafunzi kuhusu uhusiano kati ya mazingira na jamii, maji salama ni nini, na aina za takataka na jinsi ya kuzitupa. Anatumaini kwamba watoto waliofurahia kumsikiliza na kusoma juu ya mazingira wataleta mabadiliko, hata kama kidogo, kwenye maisha ya baadaye ya Tanzania.

picha

Ms. Noriko KOMATSU alikuwa muuguzi katika hospitali ya Wilaya ya Nachingwea, Lindi. Alitembelea mara kwa mara vituo vya afya vijijini Nachingwea, na kujaribu kuwafundisha akina mama njia nzuri ya kuwaangalia watoto wagonjwa. Alitambulisha kanuni ya 5S KAIZEN-TQM hospitalini, na kuchangia kwenye utunzaji na usafi wa sehemu za tiba kwa ajili ya hali nzuri ya wagonjwa hospitalini.

Ms. Norie SASAKI alifanya kazi ya elimu ya watoto wadogo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya. Alifanya kazi na walimu wa chekechea na kusisitiza umuhimu wa elimu ya watoto wadogo. Aliinua ari ya walimu wa kucheza na watoto, hivyo kukuza ndani ya watoto hisia ya ubunifu na uvumbuzi.

Mr. Hayato WATANABE alikuwa mwalimu wa ufundi magari katika Chuo cha Ufundi Songea (VETA). Alilenga kuinua uasili na ubunifu wa wanafunzi. Baada ya miaka miwili ya kazi yake, mabadiliko kadhaa yalionekana katika wanafunzi na walimu. Kwa mfano ongezeko la uwezo wa ufundi katika kazi za vitendo na ujuzi wa ufundi magari ulionekana katika wanafunzi. Vilevile walimu wenzake waliongeza ujuzi wa ufundi magari, uangalifu juu ya usalama katika kazi za vitendo na uelewa wa umuhimu wa kukarabati magari kabla ya kuharibika.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency