Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Mada na Matukio

28 Juni, 2011

Wataalam Wajapani 20 wawasili nchini Tanzania

picha

Tarehe 28 Juni, mwaka 2011, wafanyakazi wa kujitolea ishirini kutoka Japani (Japanese Overseas Cooperation Volunteers) waliwasili nchini. Watatu kati ya hawa ishirini ni walimu wa shule za msingi wenye shahada ya elimu na wataenda kufundisha katika shule zilizopo Dar es Salaam, Tanga na Iringa. Watajishughulisha zaidi kwenye masomo ya hisabati na michezo.

Kwa sasa hivi, kuna walimu wajapani 24 ambao wanafundisha hisabati na sayansi katika shule za sekondari nchini, na wengi wao wanalazimika kupambana na tatizo linalofanana ambalo linawapata wanafunzi wengi wa Tanzania, yaani upungufu wa ujuzi wa msingi wa hisabati. Hawa walimu wapya wa shule za msingi wanatarajiwa kuchangia kuinua uelewa na uwezo wa msingi wa hisabati katika ngazi ya elimu ya msingi.

Bw. Yuki Tanimura, Bi. Kasumi Kubo, na Bi. Norie Inoue ambao wataenda kufundisha shule za msingi, wanatamani kuwafundisha watoto wa Tanzania, hasa jinsi ya kuyafurahia masomo yao. "Watoto wanaweza kujifunza zaidi wakilipenda somo. Nataka wanafunzi wangu waje kufurahia hisabati, na kujihisi furaha ya uelewa," alisema Bi. Inoue mwenye uzoefu wa miaka saba ya ualimu wa shule ya msingi, Japani.

Kwa upande wake, Bw. Tanimura alisema; "ningependa kufanya kazi na walimu wa Tanzania, ili kwa pamoja tuweze kuchangia kuinua elimu ya msingi."

Bi. Kubo amefanya kazi katika shule za msingi nchini Japani kwa miaka minne, na anataka kujenga daraja nzuri la urafiki kati ya Tanzania na Japani. " Nimekuja na zawadi ndogo kutoka kwa wanafunzi wangu wa Japani kwa watoto wa Tanzania. Walizitengeneza wenyewe wakiwa wanawafikiria rafiki zao wa Tanzania ambao hawajawahi kuwaona.

Kwa kupitia programu ya wafanyakazi wa kujitolea, JICA inatarajia kuchangia maendeleo ya Tanzania, na hivyo kujenga uhusiano mzuri kati ya hizi nchi mbili ambao utasaidia kufanya maisha mazuri zaidi duniani.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency