Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Mada na Matukio

11 Novemba, 2011

Ushirikiano wa Ujuzi kati ya Akina Mama Wa-Kitanzania na Wafanyakazi wa Kujitolea kutoka Japani (9-11 Novemba, 2011)

pichaMwanakijiji na Afisa Maendeleo wa Kalenga wanaongea kuhusu VICOBA

Sisi, wafanyakazi wa kujitolea kutoka Japani (JOCV: Japan Overseas Cooperation Volunteers), tuko takribani 80 katika Tanzania nzima. Tunafanya shughuli mbalimbali kama vile ualimu wa shule za msingi, ualimu wa shule za sekondari, za ufundi, n.k. Tunaunda vikundi mbalimbali kutokana na shughuli zetu, moja ya mifano ni kikundi cha walimu kilichoundwa kwa ajili ya kuboreshe uwezo wao wa kufundisha.

Mimi ninashughulika na maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa kama Afisa Maendeleo ya Jamii. Hapa Tanzania JOCV wako wengi wanaoshughulika na maendeleo ya jamii. Baadhi yao ni Ma-Afisa Maendeleo ya Jamii kama mimi, au ni Walimu wa Vyuo. Sisi pia tunacho kikundi chetu kinachoitwa "The Community Development Group (CDG)". Tunafanya mafunzo yanayohusu maendeleo ya jamii kila mwaka ili tupate mambo mapya mbalimbali na tuboreshe uwezo wetu wa kikazi.

pichaMafunzo ya kukausha mboga

Mwaka jana, Novemba, tulifanya mafunzo katika Kijiji cha Kalenga, Wilaya ya Iringa, Mkoa wa Iringa. Lengo la mafunzo haya lilikuwa kujifunza kutoka kwa wanakijiji wa Kalenga, hasa akina mama, wanaoendelea vyema kwa kushirikiana na Halmashauri yao vizuri. Je, wanafanya shughuli gani ili wapate maisha mazuri zaidi? Hapo kijiji cha Kalenga, wanakijiji walianza kushughulikia "VICOBA(Village Community Bank)" kwa kuitikia wito wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. "VICOBA" ni mfumo wa wananchi wa akiba na mikopo vijijni. Wanakijiji wa Kalenga wanavyo vikudi sita (6) vya VICOBA kwa sasa. Kila kikundi kina Mwenyekiti, Katibu mtunzaji fedha, na Wajumbe. Kila mwanachama ananunua hisa kila wiki kutokana na uwezo wake, na baada ya miezi 3 anaweza kupata mkopo. Anayeomba mkopo anakaguliwa ndani ya chama na kama akishindwa kurudisha au akichelewa kurudisha, anatakiwa kutoa faini. Wanachama wa kijiji cha Kalenga wanaendesha VICOBA vizuri. Wanachama wakipata mikopo, wanaanza biashara. Wengine wanauza bagia, wengine wanalima na kuuza mazao au wanaendesha migahawa. Waliokopa karibu wote wamerudisha mikopo yao vizuri, yaani wanaishughulikia vizuri.

pichaWanakijiji wa Kalenga wanawafundisha wafanyakazi kutoka Japani

Kwa kuangalia shughuli zao, sisi CDG tulijifunza mengi. Kwanza tuliona kwamba akina mama wa Kalenga wanajiamini na wanajitegemea. Sasa wanachama wa VICOBA wanazo akaunti za benki mjini ili kutunza hela zao. Zamani akina mama hawakuweza kuwa na akaunti za benki lakini sasa wanaweka hela zao kwenye benki. Sasa wanaweza kuishi vizuri bila kuwategemea wanaume tofauti na zamani walivyokuwa hawana uwezo wowote bali kuwategemea waume zao tu.

Pili, tulijifunza stadi za kusuka vikapu vya kienyeji. Tulifurahi kujifunza stadi hii lakini tulishangaa ugumu wa kazi hiyo. Tuliona akina mama wa Tanzania wanayo stadi nzuri.

Wakati huo huo tulitoa mafunzo ya kukausha mboga (Dry Vegetables) kwa akina mama ili waanze kuanzisha biashara mpya ya aina hiyo. Tuliwafundisha sifa za mboga zilizokaushwa, namna ya kuzikausha na ya kuzipika. Wahudhurio walisoma vizuri na waliona kuwa wanaweza kuanzisha biashara kutumia mboga zilizokaushwa na tayari walianzisha kikundi cha VICOBA cha ukaushaji mboga mara tu walipopata mafunzo haya. Pia wahudhurio hawa waliahidi kuwa watatoa mafunzo haya kwa ajili ya wanakijiji wengine ambao hawakuhudhuria mafunzo.

Katika mafunzo haya akina CDG na wanakijiji wa Kalenga tulifundishana na tulibadilishana mawazo vizuri.Tunatamani kwamba akina mama wa Kalenga waendelee na shughuli zao vizuri zaidi na tunatamani wananchi wa Tanzania waendelee vizuri kama akina mama wa Kalenga.

picha

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency