Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Mada na Matukio

12 Aprili, 2012

Uzinduzi wa Mradi Mpya wa Maji: Kuwajengea uwezo wa DDCA ili kuisaidia sekta binafsi katika uchimbaji wa visima (12 Aprili, 2012)

PhotoDk. Hata, Mshauri Mkuu wa Mradi, na Bw. Mgaiwa, Meneja wa Mradi, wakiwa wanatoa maelezo mafupi ya mradi huo

Mwisho wa Mwezi wa Machi mwaka huu, JICA Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maji na Wakala wa uchimbaji visima na ujenzi wa mabwawa (DDCA: Drilling and Dam Construction Agency), walianzisha mradi wa Kiufundi ujulikanao kama " Mradi wa kujenge uwezo katika uchimbaji wa maji yapatikanayo chini ya ardhi" . Mkutano wa Uzinduzi rasmi wa mradi huo ulifanyika tarehe 12 Aprili mwaka wa 2012 kwenye ukumbi wa Wizara ya Maji.

Mgeni rasmi wa uzinduzi huu alikuwa Mh. Christopher Sayi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Bw. Lister Kongola, Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali za Maji, Bw. Mgaiwa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa DDCA, na Bw. Yukihide Katsuta, Mwakilishi Mkuu wa JICA Tanzania, pamoja na wataalamu wa mradi huo kutoka Japan na Wizara ya Maji.

Katika Dira ya Maendeleo ya 2025, Serikali ya Tanzania inalenga kufikisha kiwango cha upatikanaji wa maji kufikia asilimia 90 ya idadi ya watu watakaopata maji safi na salama katika maeneo ya vijijini ifikapo mwaka 2025. Taarifa ya Programu ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP) ya Program ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP) inaeleza kwamba maji yapatikanayo chini ya ardhi ni asilimia tisini na moja (91%) ya rasilimali ya maji yote kwa ajili ya usambazaji wa maji vijijini. Kwa hiyo, maendeleo makubwa ya uchimbaji wa maji yapatikanayo chini ya ardhi ni muhimu sana katika nchi ya Tanzania; Taarifa kutoka WSDP/RWSSP na ile ya Sekta ya maji zinaonyesha kwamba uwezo wa DDCA na Sekta binafsi haujafikia kiwango cha kuchimba visima elfu mbili kwa mwaka. Kutokana na hali hiyo, Serikali ya Tanzania inahitaji kuimarisha uewzo wa sekta binafsi kupitia DDCA kuwakodisha mitambo ya uchimbaji na kuwapa msaada wa kitaalamu.

Mradi huu utasaidia kuimarisha uwezo wa DDCA, Katika kitengo kipya cha kukodisha vifaa na kutoa ushauri wa kitaalamu. Inatarajia kwamba mradi huu utachangia uboreshaji wa hali ya usambazaji maji vijijini na kufikia lengo lililowekwa katika Dira ya Maendeleo ya 2025 ya Tanzania.

Kwenye mkutano huo, Mh, Christopher Sayi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, alisema kwamba; lengo la Dira ya Maendeleo ya 2025 halitaweza kufikiwa bila kushirikisha sekta binafsi. Alieleza matarajio yake katika uimarishaji na kuijengea DDCA kwa kupitia ushirikiano huu wa kitaalamu. Bw. Katsuta, Mwakilishi Mkuu wa JICA Tanzania, alisisitiza kuwa mradi huu usimamiwe na kutekelezwa vizuri na Serikali ya Tanzania ili kuweza kufikia lengo.

PhotoMh. Sayi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Bw. Katsuta, Mwakilishi Mkuu wa JICA Tanzaia, pamoja na watekelezaji wa mradi huo

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency