Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Mada na Matukio

24 Aprili, 2012

Mkutano wa Pili wa Wadau kuhusu Mpango Madhubuti wa Usafirishaji wa Shehena (24 Aprili, 2012)

PhotoBw. Motomura, Kiongozi wa Timu, alitoa maelezo ya awali juu ya mradi huu.

Kutokana na Makubaliano ya Ushirikiano wa Kitaalamu kati ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Japani (JICA) yaliyotiwa saini Mwezi Septemba mwaka 2010, mradi wa ushirikiano wa kitaalamu unaoitwa "Mradi Mtambuka wa Maendeleo ya Mifumo ya Usafirishaji na Biashara" umeanza utekelezaji tangu mwezi Agosti mwaka 2011. Mkutano wa pili wa wadau ulifanyika tarehe 24 April, 2012, jijini Dar es Salaam.

Uchumi wa Tanzania, yenye idadi ya watu zaidi ya milioni 40, umedumu katika ukuaji wa kasi katika miaka ya hivi karibuni. Katika miaka ya 2000, kasi ya ukuaji halisi imekuwa katka kiwango cha asilimia saba (7%), ambacho kinatarajiwa kuendelea kuongezeka kwa kipindi cha miaka kumi ijayo. Kwa hali hiyo, mahitaji ya usafirishaji yanatarajiwa kukua mara mbili zaidi katika kipindi kisichozidi miaka kumi ijayo. Umuhimu wa kuendeleza miundombinu unahitaji kushughulikiwa kikamilifu .

Ni muhimu kufahamu kwamba Tanzania ina njia kuu mbalimbali za usafirishaji za kimataifa zinazounganisha pwani ya Mashariki ya Tanzania na nchi jirani ndani ya bara la Afrika, na kwamba maendeleo ya miundombinu hiyo yataleta matokeo makubwa si kwa uchumi wa Tanazania tu, bali pia ukuaji wa uchumi wa nchi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki. Kutokana na mtazamo huo, miundombinu ya usafirishaji katika Tanzania inahitaji kubuniwa si kama rasilimali ya ndani tu, bali pia kama rasilimali zinazotumika pamoja kwa uchumi wa nchi jirani.

Kwa hiyo, Wizara ya Uchukuzi (Awali Wizara ya Miundombinu) imeomba Serikali ya Japani kufadhili shughuli zifuatazo;
1) Kuandaa takwimu mtambuka za usafirishaji kwa ajili ya kutengeneza mkakati wa maendeleo ya ugavi.
2) Kuandaa mpango madhubuti wa maendeleo ya usafirishaji wa shehena pamoja na miundombinu.

JICA ilianzisha mradi Agosti, mwaka 2011 kutokana na makubaliano na Serikali ya Tanzania yaliyotajwa hapo juu. Katika mradi huu, timu ya utafiti ya JICA ilifanya utafiti wa inapotokea shehena na inapofikia (ODs:origin-destination survey), na matokeo ya utafiti huu yalitumika kwa ajili ya makisio ya usafirishaji wa shehena. Matokeo yote ya utafiti na mwelekeo wa Mpango madhubuti yamewekwa kwenye taarifa ya awali ya timu ya utafiti.

Mwenyeji wa mkutano huo wa wadau alikuwa Wizara ya Uchukuzi, na katika mkutano matokeo ya utafiti pamoja na mwelekeo wa Mpango Madhubuti yaliwasilishwa. Katika mkutano huu, mashirika ya usafirishaji zaidi ya ishirini na wafadhili mbalimbali walihudhuria, na hali hiyo inaakisi hali ya utangamano iliyopo katika nyanja mbalimbali za mifumo ya usafirishaji. Baadhi ya washiriki walikuwa kutoka Wizara za Viwanda na Biashara, na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wakala wa Barabara, Mamlaka ya Bandari, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli, Askari wa Usalama barabarani.

Photo

Mada zilizotolewa na timu ya utafiti ya JICA, ziliibua majadiliano hai yenye mafanikio, kama vile umuhimu wa kujenga bandari mpya ili kupunguza msongamano kwenye bandari ya Dar es Salaam, umuhimu wa kufufua reli kwa maendeleo ya uchumi, umuhimu wa Tanzania kisiasa na kijiografia kama kitovu cha usafirishaji kwa nchi jirani zilizoko mbali na bahari.

Maoni na mapendekezo yaliyotolewa na wadau yatajumuishwa katika rasimu ya mpango madhubuti itakayo wasilishwa mwezi Septemba, mwaka huu.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency