Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Mada na Matukio

30 Juni, 2017

TRA na JICA zimesaini makubaliano ya ushirikiano katika Mradi wa kiufundi kwa ajili ya kuboresha Usimamizi wa Kodi

Katika Juhudi za kusaidia ukusanyaji wa mapato, Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani (JICA) limeingia katika makubaliano ya kusaidia Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) kuongeza uwezo wa Mamlaka hiyo kukusanya kodi kupitia Mradi wa Ushirikiano wa Kiufundi kulingana na utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa Miaka Mitano Tano (2016 / 17 mpaka 2020 / 21). TRA kama nguzo muhimu katika juhudi za ukusanyaji wa mapato ya ndani imekua mstari wa mbele katika kuongeza uwezo wa wafanyakazi wake katika usimamizi wa kodi. Ili kufikia lengo hili, TRA inashirikiana na JICA kupitia mradi mradi huu inawajengea wafanyakazi wa ngazi mbalimbali wa TRA uwezo wao wa kiufundi kwa kushirikiana na wataalam wa kodi kutoka JICA.

Kuanzia 2012 mpaka 2016, TRA na JICA zilitekeleza mradi wa kwanza na kufanikiwa kuimarisha uwezo wa Chuo cha Kodi (ITA) ikiwa ni pamoja na marekebisho ya Kozi ya Msingi ya Kodi (Taxation Basic course) na kuafanikisha kuunda kozi mpya kama kozi ya juu ya Kodi yaani Taxation Advanced Course, Electronic Accounting System course International Taxation course na pia kuandaa Warsha juu ya Extractive Industry. Katika mradi wa kwanza, TRA ilitoa mafunzo kwa maafisa wa kodi 390 (mpaka kufikia Aprili 2016) kwa kushirikiana na JICA na Mamlaka ya Kodi ya Japani (NTA).

Kutokana na mafanikio hayo, mnamo Novemba 2016, Mamlaka ya Mapato Tanzania na JICA zilifanya mazungumzo ya pamoja pamoja na kufanikiwa kuunda mradi mwingine wa awamu ya pili . Baada ya mazungumzo hayo tarehe 29 Juni 2017, Bw Charles E. Kichere, Kamishna Mkuu wa TRA na Bw Toshio Nagase, Mwakilishi mkuu wa JICA Tanzania, walisaini Kumbukumbu ya Majadiliano (Recoerd of discusion R / D) kuelekea kuanza kwa Mradi.

Mradi unalenga kuziba pengo la ujuzi kwa maafisa wa kodi ili kuiongezea Uwezo Mamlaka ya Mapato Tanzania. Mradi huu mpya utashughulika na maeneo makuu matatu: (1) Kwa kuhuisha na kuboresha mafunzo yanayotolewa na Chuo cha Usimamizi wa Kodi [ITA], (2) Kusaidia juhudi za TRA katika kuunda mfumo wa Mafunzo Kazini na (3) kufafanua kwa undani mfumo wa kujenga/kuendeleza mfumo wa ujuzi na utaalam wa wafanyakazi (career development). Shughuli hizi zinaingiliana na zitatengeneza msingi wa maendeleo ya wafanyakazi ili kufikia uboreshaji endelevu na kuongeza mapato ya ndani.

Mradi unatarajiwa kuanza mwezi Agosti au Septemba 2017 na utatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu mfululizo

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency