Aina | Eneo | Muda | Shirika la Tanzania | Gharama (Yen Mill.) |
---|---|---|---|---|
Ruzuku | Pwani, Dar es salaam | Julai 2007- Machi 2009/ Juni 2008-Machi 2010 |
Wizara ya Maji na Umwagiliaji | 818/ 887 |
Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, ambayo inajumuisha mji mkuu wa Dar es Salaam, ni mikoa inayokua kwa kasi na inayotarajiwa kuendelea kupata maendeleo. Hata hivyo, kutokana na sensa ya idadi ya watu ya mwaka 2002, kiwango cha upatikanaji wa maji salama katika mikoa hii ni asilimia 23 tu.
Ili kuboresha hali hiyo mbaya ya maji, katika mradi huu vijiji 13 vilitengenezewa mifumo ya maji ya bomba, wakati vjiji vingine saba vilitengenezewa mifumo 22 ya maji yenye pampu za mkono. Msaada huu utaboresha zaidi kiwango cha maisha ya jamii za wenyeji kwa kuwapa maji salama watu elfu 46 na angalau kuhakikisha usambazaji wa maji salama kwa asilimia 66 ya mikoa hii ifikapo mwaka 2015.
scroll