Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Shughuli katika Tanzania

Program ya Wajapani wa Kujitolea Tanzania (JOCV)

Photo

Programu ya Wajapani wa kujitolea wa JICA (JOCV) ilianza mnamo mwaka1965. Hadi kufikia sasa, zaidi ya wajapani wa kujitolea 54,000 wametumwa kufanya kazi pamoja na jamii za wenyeji katika nchi 98 na sehemu mbalimbali duniani. Programu hii inakusudia kufikia malengo yake makuu matatu kama ifuatavyo:

 1. Kushirikiana kwenye maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na pia ujenzi wa nchi zinazoendelea
 2. Kukuza ushirikiano, kuishi pamoja na kuelewa tamaduni za jamii husika
 3. Kurudisha uzoefu wa kujitolea kwa jamii

Kundi la kwanza la Wajapan wa kujitolea (JOCV) liliwasili Tanzania mnamo mwezi Machi 1967. Lilikuwa kundi la pili kupelekwa Afrika. Tangu wakati huo, wataalam hao wa kujitolea wapatao 1,700 hivi wameshatumwa Tanzania. JOCV wanaishi na kufanya kazi na wanajamii wakizungumza lugha moja (yaani Kiswahili) kama jamii za wenyeji na kufanya shughuli kwa malengo ya kujitegemea na kupata mabadiliko endelevu.

Programu ya JOCV nchini Tanzania inazingatia maeneo matatu ya kipaumbele:

 1. Kukuza ukuaji wa uchumi
 2. Kukuza maendeleo ya miundombinu yanayopelekea maendeleo ya kiuchumi wa kijamii
 3. Kuboresha utawala na utoaji wa huduma bora kwa umma

JOCV wamefanya kazi katika maeneo mbalimbali ya Tanzania, yakiwa ni pamoja na jiji kubwa zaidi (Dar es Salaam), eneo la ndani (Morogoro, Iringa na Dodoma), eneo la pwani ya Bahari ya Hindi (Bagamoyo, Pwani, Tanga), ukanda wa Mlima Kilimanjaro, ndani ya jiji la Ziwa Victoria (Mwanza), maeneo ya nyanda za juu (Mbeya na Ruvuma), mpakani mwa Msumbiji (Mtwara na Lindi), na Zanzibar.

JOCV kwa ujumla hufanya kazi kwa miaka miwili, na JICA huwapatia mafunzo ya lugha ya Kiswahili nchini Japan na Tanzania kabla ya kwenda kuanza kazi zao, kwani wanafanya kazi ndani na wananajamii wa Tanzania kwa maendeleo ya kuinua uchumi.

JOCV wanafanya kazi katika nyanja zifuatazo nchini Tanzania:


Maeneo ya Kipaumbele: Kukuza Ukuaji wa Uchumi
Eneo: Kilimo

PhotoJOCV wa kilimo cha mbogamboga akitoa mwongozo wa kilimo bora

Sekta ya kilimo nchini Tanzania huchangia karibu robo ya pato la Taifa, na karibu asilimia 80 ya watu wanaishi kutokana na kilimo, ambacho ndio msingi wa ukuaji wa uchumi wa nchi. Hivyo, JICA inatekeleza misaada mingi kupitia miradi ya misaada nafuu na ile ya ushirikiano wa kiufundi katika nyanja hii ya kilimo. Kwa kupitia mpango huu wa wataalam wa kujitolea, JICA imetuma wataalamu hao katika eneo la kukuza mazao ya mbogamboga na ufugaji.


Maeneo ya Kipaumbele: Kukuza Vyanzo vya Kuendesha Uchumi
Eneo: Maendeleo ya Rasilimali Watu

PhotoMwalimu wa Kompyuta akifundisha wanafunzi jinsi ya matumizi bora ya kompyuta

Nchini Tanzania, ambapo ukuaji mkubwa wa uchumi unaendelea, maendeleo katika rasilimali watu katika tasnia ya teknolojia inahitajika sana. JOCV wengi wamefanya kazi katika vituo maalumu vya mafunzo ya ufundi, vyuo vikuu na taasisi zingine za elimu ya juu ili kuchangia katika maendeleo ya rasilimali watu. Katika vituo vya mafunzo ya ufundi, JOCV wamefanya kazi katika eneo la Kompyuta na nyanja zake kwa kushirikiana na vyuo mbalimbali japo JOCV wa TEHAMA (ICT) wamepelekwa taasisi za elimu ya juu kama vile vyuo vikuu ili kukidhi mahitaji ya mahali hapo.


Maeneo ya Kipaumbele: Uboreshaji wa Utawala na Utoaji wa Huduma za Umma
Sekta: Elimu

PhotoJOCV akiwa darasani akifundisha hisabati katika shule ya sekondari

Ili kuongeza huduma za umma katika sekta ya elimu Tanzania, kuna maombi mengi ya JOCV katika elimu ya sayansi na hisabati na pia katika shule za msingi. JOCV wa elimu ya sayansi na elimu ya hisabati hufundisha katika shule za sekondari kutokana na uhaba wa muda mrefu wa walimu wa sayansi na hisabati ambapo ni moja ya changamoto kubwa nchini Tanzania inayosababisha wanafunzi kutoendelea vizuri katika elimu ya sekondari. JOCV wa shule za msingi na wale walio katika shule za sekondari wakati mwingine hushirikiana ili kuchangia katika kuboresha maarifa na ujuzi wa kimsingi wa wanafunzi wao.


Maeneo ya Kipaumbele: Uboreshaji wa Utawala na Utoaji wa Huduma za Umma
Sekta: Usimamizi wa Serikali za Mitaa

PhotoJOCV wa maendeleo ya jamii akisaidia katika shughuli za kijamii

Hii sekta inahusu kuwajengea uwezo wa usimamizi wa fedha za umma, ambao ni moja ya masuala ya maendeleo nchini Tanzania. Mpango wa kujitolea unasaidia kuleta mageuzi ya serikali za mitaa, hasa katika maendeleo ya jamii. JOCV wanafanya kazi za maendeleo ya jamii ili kurahisisha uboreshaji wa ufanisi wa kazi katika halmashauri za wilaya, manispaa na miji na baadhi ya maeneo mengine kwenye serikali za mitaa. Wanachangia pia katika kuwajengea uwezo wafanyakazi katika serikali hizo za mitaa na mara nyingi hufanya kazi na wanajamii wa eneo husika, hasa wanawake kwa kuhamasisha shughuli zao.


Maeneo ya Kipaumbele: Uboreshaji wa Utawala na Utoaji wa Huduma za Umma
Sekta: Afya

PhotoJOCV katika sekta ya Uuguzi akikuza 5S-KAIZEN hospitalini

Ili kujenga uwezo na kukuza usimamizi wa fedha za umma nchini Tanzania kwa ujumla, JOCV wamefanya kazi katika nyanja hii ya huduma ya afya ya umma. JOCV katika nyanja za uuguzi na ukunga wamepelekwa kufanya kazi katika hospitali kwenye vitengo maalumu ikiwa ni pamoja na hospitali za kitaifa, mkoa na wilaya. JOCV wa uuguzi na ukunga wamesaidia kuwezesha shughuli za 5S-KAIZEN (yaani, usimamizi wa ubora) ili usimamizi wa ubora uanzishwe katika maeneo yao waliyopewa. JOCV wamechangia sana katika halmashauri za manispaa na wilaya kwa kuwajengea wafanyikazi uwezo. Utaalamu wa viungo ni eneo lingine ambalo JOCV wanapangiwa hospitali kutoka ngazi ya kitaifa hadi wilaya. Moja ya shughuli za kujitolea katika eneo hili ni kutoa ushauri juu ya matibabu ya wagonjwa kupitia kazi zao, na wenzao wa Kitanzania, ambayo hufanya uboreshaji wa ustadi wa wataalamu wa tiba nchini Tanzania.


Maeneo ya Kipaumbele: Uboreshaji wa Utawala na Utoaji wa Huduma za Umma
Sekta: Elimu ya Viungo, Michezo

PhotoJOCV wa baseball akifundisha vijana

JICA imetuma wataalamu wa kujitolea (JOCV) kufundisha elimu ya viungo (P.E.) kwa taasisi za sekondari na elimu ya juu kwa lengo la kueneza elimu hiyo hasa katika mchezo wa baseball nchini Tanzania. Kwa kuongezea, kulingana na mpango wa 'SPORTS FOR TOMORROW (yaani, MICHEZO KWA AJILI YA KESHO)' ulioasisiwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Japani, Shinzo Abe, JICA imetoa nafasi nyingi kwa Watanzania kushiriki katika shughuli za michezo. Mbali na elimu ya viungo, JICA imetuma wataalam wa baseball wa kujitolea na judo nchini Tanzania.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency