Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Shughuli katika Tanzania

Maendeleo ya Kilimo na Maendeleo ya Vijijini

Sekta ya kilimo inachangia kiasi cha asilimia 20 ya bidhaa zinazosafirishwa nje ya nchi, zaidi ya asilimia 40 ya pato la taifa (GDP) na pia inasaidia riziki ya theluthi mbili ya familia nchini Tanzania. Kilimo kinachukua sehemu muhimu katika kukua kwa uchumi na kupunguza umaskini. Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA) pia unalenga kukuza sekta ya kilimo hadi kufikia kiwango cha ukuaji asilimia 10 kwa mwaka.

Hata hivyo, kuna vikwazo vya aina mbalimbali mfano, pembejeo zisizotosheleza kama vile mbegu bora, mbolea na dawa za kilimo, mfumo wa kizamani wa uoteshaji mazao na ucheleweshaji wa maendeleo ya miundombinu kama vile, skimu za umwagiliaji, miundombinu ya masoko, barabara za mashambani, upelekaji wa umeme vijijini na usindikaji wa mazao.

Kwa utekelezaji mzuri wa Mipango ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP), Japan inasaidia kujenga uwezo katika upangaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADPs) na katika ufuatiliaji na tathmini (M & E) katika ngazi ya serikali kuu na serikali za mitaa. Kwa kuzingatia “Muungano wa Maendeleo ya Kilimo cha Mpunga Afrika (CARD)”, ambao ulizinduliwa katika Mkutano wa Nne wa Tokyo wa Kimataifa kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD IV), misaada inayohusiana na CARD inafanyika kupitia mafunzo ya wakulima viongozi, kuimarisha utafiti na uendelezaji, na uboreshaji wa mbinu za kilimo cha mpunga katika muundo wa ASDP.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency