Japan International Cooperation Agency
Share
  • 日本語
  • English
  • Français
  • Espanol
  • Home
  • About JICA
  • News & Features
  • Countries & Regions
  • Our Work
  • Publications
  • Investor Relations

Shughuli katika Tanzania

Kuimarisha Uwezo wa Kusaidia uanzishaji na utekelezaji wa DADPs (Mipango ya Maendeleo ya Kilimo Wilayani)

Aina Eneo Muda Shirika la Tanzania Gharama (Yen Mill.)
Ufundi Nchi nzima Machi 2009-
Machi 2012
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika 230

pichaMkutano wa tathmini ya DADPs uliofanyika wizarani

Mradi huu wa Ushirikiano wa kiufundi ni sehemu moja ya misaada inayofuata “Programu ya kusaidia Sekta ya Maendeleo ya Vijijini na Kilimo” ambayo ilisaidiwa na Japani na iliisha mwezi Februari 2009. Asilimia sabini na tano ya bajeti ya serikali kuu ya Tanzania kwa ajili ya sekta ya kilimo imetengwa kwa ajili ya maendeleo katika ngazi ya wilaya. Mradi huu ulianzishwa kusaidia utekelezaji wa zoezi la kuleta maendeleo haya.

Malengo ya mradi ni kuanzisha na kutekeleza Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADPs) ambayo ni kipengele cha awali katika Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP) inayojumuisha shughuli zote za kilimo nchini Tanzania, na pia kuimarisha mfumo wa kusaidia utekelezaji wa DADPs.

Yapo matarajio makubwa kwamba sekta ya kilimo Tanzania italeta maendeleo ya uchumi, itapunguza umaskini na kuhakikisha upatikanaji wa chakula cha kutosha. Ingawaje juhudi kubwa zimefanyika kuanzisha ASDP, swali lililopo sasa ni jinsi gani ya kufanya ili programu hii ifanikiwe kuleta maendeleo ya kweli.

Timu ya mradi inajumuisha mshauri mkuu, ambaye alihusishwa katika “Programu ya kusaidia Sekta ya Maendeleo ya Vijijini na Kilimo”, pamoja na wataalamu wanne wa JICA. Timu inafanya kazi kwa karibu na wenzao kutoka serikali ya Tanzania ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.

(Rejea)
DADPs inaweka umuhimu katika shughuli za ngazi ya chini. Asilimia 75 ya bajeti ya ASDP hupelekwa wilayani kwa kuzingatia DADPs. Ushirikiano huu wa kiufundi wa JICA una madhumuni ya kuimarisha uanzishaji na utekelezaji wa DADPs.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency