Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Shughuli katika Tanzania

Kuongeza uwezo kwa Mifumo ya Ufuatiliaji na Tathmini ya ASDP (Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo)

Aina Eneo Muda Shirika la Tanzania Gharama (Yen Mill.)
Ufundi DSM, Morogoro, Dodoma Machi 2008- Machi 2011 Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika 330

pichaKamati ya utendaji ya M&E na staff za mkoa wanaongea juu ya ukusanyaji wa takwimu

Ili kuthibitisha matokeo ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP) ambayo ilianza mwaka 2006, ni muhimu kupata taarifa za maeneo husika kupitia mifumo ya Ufuatiliaji na Tathmini (M & E) na kujua mwelekeo katika maendeleo ya kilimo. Kwa bahati mbaya, kwa kuwa mfumo uliopo wa serikali kuu wa ukusanyaji na utoaji wa ripoti kutoka vijijini hautoshelezi, ripoti za maeneo stahiki (kwa mfano zile za mavuno ya mazao au idadi ya mifugo) mara nyingi hazifikii zile wizara zinazohusika za sekta ya kilimo.

Lengo la mradi huu ni kuboresha mfumo wa utoaji taarifa kwa vipindi maalumu kwa ajili ya takwimu za kilimo kati ya vijiji na serikali, na pia uongezaji wa uwezo wa watumishi kwa ajili ya utendaji. Wizara tano zinazofanya kazi katika sekta ya kilimo zinashiriki katika kamati ya utendaji ya M&E ya ASDP ili kuunganisha mahitaji yao ya takwimu na kutayarisha rasimu ya muundo iliyofanana itakayotumika wakati wa kuwasilishwa ripoti kutoka vijijini hadi kwenye wizara husika. Mradi huu unauboresha mfumo wa utoaji taarifa kwa kupitia majaribio, na mafunzo na maelekezo kwa watumishi husika katika wilaya nne za mikoa ya Morogoro na Dodoma kabla ya hitimisho.

Kushiriki kwa JICA katika ushirikiano huu wa kiufundi kunahusisha kupeleka timu ya washauri wanne katika mradi huu ambao wameanzisha ofisi yao katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ili kushirikiana na kamati ya utendaji ya M&E.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency