Aina | Eneo | Muda | Shirika la Tanzania | Gharama (Yen Mill.) |
---|---|---|---|---|
Ufundi | Morogoro, Kilimanjaro, Mbeya, Mtwara |
Feb. 2007 – Jan. 2010 |
Wizara ya maji na umwagiliaji | 340 |
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ameyapa kipaumbele maendeleo ya umwagiliaji. Kutokana na hilo, serikali ya Tanzania imekuwa ikipanua wigo wa umwagiliaji katika kiwango cha wastani kwa zaidi ya hekta elfu 16 kwa mwaka hivi karibuni. Kufuatia mfumo wa kupeleka madaraka mikoani tangu mwaka 2002, jukumu la kuanzisha skimu mpya za umwagiliaji wa mashamba madogo na kuboreshwa kwa miundombinu iliyopo limehamishiwa katika ngazi ya wilaya. Kwa bahati mbaya, wahandisi wengi wa umwagiliaji wa wilaya hawana uzoefu na wanakosa miongozo sahihi ya kazi. Kwa hiyo, miongozo ya wahandisi hao inahitajika ili kuhakikisha kwamba maendeleo ya umwagiliaji yanafanikiwa na kuwa endelevu.
Wataalamu wa JICA pamoja na ofisa wa Umwagiliaji katika ofisi ya kanda ya Mbeya
JICA inafanya kazi ya kuimarisha uwezo wa wahandisi wa umwagiliaji katika kanda na wilaya kwa kutoa mafunzo ya vitendo katika miundombinu iliyopo na inasaidia kuandaa miongozo ya kusaidia uanzishaji wa skimu mpya. Katika utunzaji wa miundombinu, JICA, kwa kuzingatia uwezo wa jamii za wakulima, inajaribu kupunguza misaada ya kifedha na vifaa inayotoka nje. Huku kuhamishwa kwa ujuzi, pamoja na usaidizi wa wataalamu wawili wa JICA, kutaifanya Tanzania kuwa taifa linalojitegemea katika kilimo.
scroll