Japan International Cooperation Agency
Share
  • 日本語
  • English
  • Français
  • Espanol
  • Home
  • About JICA
  • News & Features
  • Countries & Regions
  • Our Work
  • Publications
  • Investor Relations

Shughuli katika Tanzania

Kusaidia Mifumo ya Utoaji Huduma ya Kilimo cha Umwagiliaji (Tanrice)

Aina Eneo Muda Shirika la Tanzania Gharama (Yen Mill.)
Ufundi Nchi Nzima Juni 2007- Juni 2012 Wizara ya Kilimo, chakula na ushirika 655

pichaUfundi uliofundishwa kwenye mafunzo (Mistari iliyonyooka ya upandaji na mashine ya kupalilia)

Uzalishaji wa mpunga nchini Tanzania unashindwa kuendana na ongezeko la sasa la mahitaji, hivyo, inabidi kuagiza mpunga kutoka nje ili kutosheleza mahitaji. Japani imekuwa inatoa misaada yake kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji nchini Tanzania tangu miaka ya 1970, kwa kuanzia katika Wilaya ya Moshi Vijijini huko Mkoani Kilimanjaro. Kutokana na ushirikiano huu, mavuno ya mpunga tayari yamefikia tani sita kwa hekta, kiwango ambacho ni juu ya kile cha taifa ambacho ni tani mbili kwa hekta. Tangu miaka ya 1990, ili mafanikio haya yasambae nchi nzima, JICA imekuwa inasaidia kuboresha uzalishaji wa mpunga kwa kuwapa mafunzo zaidi ya wataalamu na wakulima wa umwagiliaji elfu moja, kuanzishwa na kutekeleza mbinu mpya za mafunzo ya kilimo ambazo zinawanufaisha wakulima moja kwa moja katika kanda sita za mfano za umwagiliaji.

Lengo la mradi ni kuhakikisha kuwa mbinu hizi zinaanzishwa katika vituo vingine vitatu vya mafunzo ya kilimo ili kusaidia kuongezeka kwa mapato ya mpunga na hivyo kuboresha hali ya maisha kwa jamii za vijijini Tanzania. Wakulima ambao wamepata mafunzo wanatakiwa kuwashirikisha wengine ujuzi walioupata. Mafunzo yanajumuisha mbinu muhimu za kilimo zenye gharama ndogo, kama usimamizi wa kutunza matuta, usawazishaji wa ardhi, upandaji katika mistari iliyonyooka, na matumizi ya mashine ya kupalilia iliyotengenezwa kwa mkono. Aidha, mafunzo yanafanyika kwa kuzingatia usawa wa jinsia kwa kuhimiza ushiriki wa asilimia hamsini kwa hamsini baina ya wanaume na wanawake.

Lengo kubwa la mradi ni kusambaza mafunzo haya katika kanda 40 za umwagiliaji nchini katika kipindi cha miaka mitano ya ushirikiano. Msaada mwingine ni kuboresha uzalishaji wa mpunga si wa ardhi tepe tu, bali wa ardhi kavu kwa kusaidia uchaguaji wa aina ya mpunga ulioboreshwa pamoja na Mpunga Mpya kwa Afrika (NERICA).

Ushiriki wa JICA katika ushirikiano huu wa kiufundi unahusisha upelekaji wa wataalamu wanne ambao watashirikiana na wenzao wa Tanzania ili kuhakikisha mafanikio ya mradi.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency