Japan International Cooperation Agency
Share
  • 日本語
  • English
  • Français
  • Espanol
  • Home
  • About JICA
  • News & Features
  • Countries & Regions
  • Our Work
  • Publications
  • Investor Relations

Shughuli katika Tanzania

Utawala

Katika muktadha wa misaada wa kimaendeleo, "utawala" unamaanisha "uwezo wa serikali kusimamia au kuongoza nchi". Nchi za Afrika kwa ujumla zina serikali dhaifu, na Tanzania ni miongoni mwa nchi za namna hiyo. Utoaji wa msaada kwa tawala husika unaongeza uwezo wa nchi hiyo kujiendesha yenyewe, kuharakisha mchakato wa kujitawala, na mwishowe huongeza kiwango cha kuaminiwa kwa nchi hiyo na jumuiya ya kimataifa.

Kwa kuwa utawala unajumuisha maeneo mengi ikiwa ni pamoja na mfumo wa sheria, uundwaji na utekelezaji wa sera na serikali za mitaa, hali ya utawala nchini Tanzania haiwezi kuelezwa kwa urahisi kwa muhtasari katika taarifa fupi. Kwa mfano, kwa kuangalia katika Jedwali la orodha ya utawala ya mwaka 2009 ambayo iliyotolewa na Benki ya Dunia, Tanzania iliorodheshwa mwishoni mwa asilimia za katikati katika uwajibikaji wa serikali. Katika kupanga viwango vya rushwa duniani vya mwaka 2009, vinavyotolewa kila mwaka na Asasi ya Kimataifa isiyo ya Kiserikali (Transparency International) Tanzania iliwekwa kwenye nafasi ya 116 kati ya mataifa 180 ambapo nafasi ya juu iliashiria kuwa kuna rushwa kidogo.
(*Japani ilikuwa kwenye nafasi ya 18 katika viwango vya rushwa duniani).

Mpaka sasa utoaji wa huduma za umma na za ustawi wa jamii kwa wananchi kwa ujumla haukufanywa kwa kiwango cha kuridhisha katika nchi hii kutokana na Serikali Kuu kutokuwa na uwezo wa kuratibu pamoja na ukosefu wa uwezo wa Serikali za Mitaa katika kutekeleza huduma hizo.

Mwaka 2005, Serikali ya Tanzania ilianzisha Mkakati wake wa Kitaifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA). Moja ya mihimili ya MKUKUTA ni kuimarisha utawala bora kwenye serikali kuu pamoja na serikali za mitaa, na ili kufikia lengo hilo serikali imezindua mfululizo wa marekebisho ya kiutawala. Japani imekuwa ikitoa msaada katika eneo hili kwa kuweka mkazo maalumu katika eneo la "marekebisho ya serikali za mitaa" na "marekebisho ya usimamiaji wa fedha za umma".

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency