Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Shughuli katika Tanzania

Ushirikiano wa Kiufundi katika Kuimarisha Mpango Shirikishi na Mzunguko wa Maendeleo ya Kijamii kwa Utawala Bora wa Serikali za Mitaa

Aina Eneo Muda Shirika la Tanzania Gharama (Yen Mill.)
Ufundi Pwani Morogoro Oktoba 2009 – Oktoba 2014 Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 350

picha

Ili kuakisi sauti za watu katika kuandaa mpango wa maendeleo kwenye serikali za mitaa, mfano wa maendeleo shirikishi umekuwa ukitumiwa katika sehemu za vijijini nchini Tanzania; mfano huu unajulikana kama Fursa na Vikwazo katika Mchakato wa Maendeleo (O&OD). Mbinu hii ni ya kipekee kwa Tanzania na imeshaanzishwa katika wilaya zote 133 kuanzia mwaka 2002.

Kulikuwa na kazi zilizofanyika kabla ya kuanza mradi huu. "Utafiti kuhusu uboreshaji wa Fursa na Vikwazo katika Mchakato wa Mpango wa Maendeleo" ulifanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na JICA kutoka mwaka 2006 hadi 2008. Utafiti huo ulipendekeza kuwa utaratibu wa O&OD ni mzuri na una umuhimu wake katika kuendeleza utawala bora ikiwa utaboreshwa kidogo. Kutokana na utafiti huu, mradi huu umeanzishwa ukijumuisha mapendekezo hayo na kuonekana kama awamu ya kwanza ya kuweka msukumo katika mfano wa O&OD ulioboreshwa. Malengo ya mradi ni kwanza kabisa kuanzisha mfumo wa kutoa mafunzo kwa viongozi wa serikali za mitaa ambao watapata mafunzo ili kufanya kazi muhimu ya "mwezeshaji" katika mchakato wa maendeleo, na pili ni kuwa na mfano unaofaa kupitia shughuli za kuongoza za O&OD iliyoboreshwa katika vijiji 10 ndani ya wilaya 5 za mikoa ya Pwani na Morogoro.

Shughuli za mradi huu zinafanywa na wataalamu wanne wa JICA ambao wanafanya kazi pamoja na watumishi kutoka OWM-TAMISEMI kama wenzi wao katika kazi.

Viungo Vihusikavyo

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency