Mshauri wa Utawala wa Serikali za Mitaa

Aina Eneo Muda Shirika la Tanzania Gharama (Yen Mill.)
Ufundi Dodoma Septemba 2010 - Septemba
2012
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 40

Mshauri wa utawala wa serikali za mitaa anatarajiwa kuinua ufahamu wa viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), na Ofisi za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kupitia ushauri wake juu ya maendeleo ya marekebisho ya serikali za mitaa na mifumo ya serikali za mitaa na kadhalika.

picha

JICA imekuwa inaleta mshauri wa serikali za mitaa kwa TAMISEMI tangu mwaka 2002, na mtaalamu wa sasa hivi, Bw. Michiyuki Shimoda, ni wa pili. Yeye anafanya kazi si ya kiushauri tu, bali pia, anafanya kazi ya uratibu wa miradi mbalimbali ya JICA na pia kusimamia Programu ya Pili ya Marekebisho ya Serikali za Mitaa ambayo inaendeshwa na Serikali ya Tanzania.