Aina | Eneo | Muda | Shirika la Tanzania | Gharama (Yen Mill.) |
---|---|---|---|---|
Ufundi | Dar es Salaam | Octoba 2009 - Octoba2012 | Wizara ya Fedha | 200 |
Serikali ya Tanzania kwa kupitia Wizara ya Fedha imekuwa inatekeleza Programu ya Marekebisho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP) kutoka mwishoni mwa miaka ya tisini kwa msaada wa wabia wa maendeleo. Japani ilitoa msaada wa awali wa "usimamizi wa fedha na utunzaji hesabu" ambao ni kipengele kilicho katika awamu ya pili ya PFMRP kuanzia mwaka 2004. Kati ya mwaka 2005 na 2007, uimarishaji wa uwezo wa usimamizi wa fedha za umma na uhamasishaji wa PFMRP ulifanywa kupitia Utafiti wa Maendeleo uliofanywa na JICA kupitia msaada ulioitwa "Msaada wa Kujenga Uwezo katika usimamizi wa Fedha za Umma". Awamu ya tatu ya utafiti huo ilianza Julai 2008, ambayo iliyapa kipaumbele maeneo ya uimarishaji wa mfumo wa ndani wa ukaguzi wa hesabu za serikali kuu na serikali za mitaa.
Kitengo Kikuu cha Ukaguzi wa Ndani wa Hesabu (CIAU) kilianzishwa kwenye Idara ya Mhasibu Mkuu ya Wizara ya Fedha ili kutoa msaada kwa ajili ya kusimamia na kuimarisha uwezo wa ofisi za ukaguzi wa fedha wa ndani za Serikali Kuu na Serikali za Mitaa. CIAU inahitaji kuimarisha uwezo wake wa kutoa mwongozo unaotosheleza, usimamizi na mafunzo ili kuboresha kazi za ukaguzi wa hesabu za fedha wa ndani wa serikali ya Tanzania. Ili kushughulikia changamoto ambazo CIAU inakumbana nazo na mapendekezo ya utafiti wa maendeleo wa awali; wataalamu watatu wa JICA wanafanya kazi na watumishi wenzao wa CIAU wakiwa na lengo la kuimarisha uwezo wa CIAU.
scroll