Japan International Cooperation Agency
Share
  • 日本語
  • English
  • Français
  • Espanol
  • Home
  • About JICA
  • News & Features
  • Countries & Regions
  • Our Work
  • Publications
  • Investor Relations

Shughuli katika Tanzania

Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Mafunzo ya Serikali za Mitaa (Awamu wa Pili)

Aina Eneo Muda Shirika la Tanzania Gharama (Yen Mill.)
Ufundi Dodoma Julai 2011 - Julai 2015 Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 370

pichaManispaa ya Wilaya ya Manyoni

Mwaka 1998, Utaratibu wa Upelekaji Madaraka Mikoani (D by D) ulianzishwa Tanzania kwa kuhamisha madaraka ya kisiasa, kifedha na kiutawala kutoka serikali kuu kwenda kwenye mamlaka za serikali za mitaa na hatimaye kwa watu wa Tanzania. Pamoja na jitihada nyingi zilizofanyika katika kipindi cha miaka kumi uwezo wa serikali za mitaa zipatazo 133 unabaki kuwa ni kikwazo mpaka sasa. Kuna tofauti kubwa kati ya kilichotarajiwa na kilichoko sasa.

Mwaka 2008, JICA ilikubali maombi kutoka Serikali ya Tanzania ya kusaidia jitihada za kuimarisha uwezo wa wafanya kazi wa Serikali za Mitaa, na hivyo kuanza kutoa msaada wa kiufundi kupitia Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Mafunzo ya Serikali za Mitaa.

Wakati wa ushirikiano huo kati ya mwaka 2008 na 2010, JICA iliisaidia TAMISEMI katika uratibu wa maoni mbalimbali kutoka wadau wa nyanja nyingi kwa kuanzisha Kikosi Kazi ambacho kilipewa jukumu la kuandaa mkakati wa kueleweka wa mafunzo.

"Mkakati wa Mafunzo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa" ya TAMISEMI unaeleza mambo mbalimbali yakiwemo uhusiano baina ya mahitaji halisi ya mafunzo na kiwango cha utekelezaji, utaratibu mzuri wa kupeleka pesa za msaada kuimarisha uwezo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, na uanzishwaji wa mfumo wa utoaji wa mafunzo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Utekelezaji wa mkakati huu ulianza mwaka 2010 na kupanuka zaidi mwaka 2011. Ili kuhakikisha kwamba Mkakati huo wa Mafunzo unatekelezwa kikamilifu, inatambuliwa kwamba mchango wa Taasisi Kiongozi ya Mafunzo (LTI) haya itakuwa muhimu sana. Hii ni kwa sababu chini ya mpango mpya wa mafunzo Taasisi hiyo imepewa jukumu maalum la kuratibu mafunzo yote yanayotolewa kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Taasisi ya Mafunzo ya Serikali za Mitaa (LGTI) ilichaguliwa kama Taasisi Kiongozi ya Mafunzo, na TAMISEMI na LGTI kwa pamoja ziliiomba JICA kusaidia kuimarisha uwezo wa LGTI kwa kupitia mradi huu ili taasisi hiyo iweze kufanya kazi kikamilifu na kutimiza mujukumu yake vizuri. Mradi huu wa Kuimarisha Uwezo wa Mafunzo ya Serikali za Mitaa (Awamu wa Pili) utaanzisha mifumo ya uratibu wa mafunzo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na mafunzo yanayotolewa na watu mbalimbali, pamoja na kuthibiti ubora wa mafunzo hayo.

Kwa sasa hivi kuna wataalamu wawili wa JICA pamoja na wenzi kazi wao kutoka LGTI na TAMISEMI ambao kwa pamoja wanafanya kazi katika mradi huu huko Hombolo, Dodoma.

Viungo Vihusikavyo

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency