Japan International Cooperation Agency
Share
  • 日本語
  • English
  • Français
  • Espanol
  • Home
  • About JICA
  • News & Features
  • Countries & Regions
  • Our Work
  • Publications
  • Investor Relations

Shughuli katika Tanzania

Mfuko wa Pamoja na Msaada wa Maendeleo ya Serikali za Mitaa (LGDG)

Aina Muda Shirika la Tanzania Gharama (Yen Mill.)
Ruzuku Julai 2008 - Juni 2012 Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 100

Kama sehemu ya mchakato wa upelekaji wa madaraka mikoani, Serikali ya Tanzania imeanzisha mfumo wa msaada wa fedha, ambao unaziruhusu Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia, kulingana na vipaumbele vya maendeleo vya Mamlaka hizo, fedha ambazo zinapelekwa huko bila masharti mengine. Mfumo wa Mfuko wa pamoja ulianzishwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wabia wa maendeleo pamoja na Benki ya Dunia. Katika mfuko huo Japani ilichangia Yen milioni 100 kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitatu tangu mwaka 2008. Kiasi kinachotengwa kwa kila Mamlaka ya Serikali ya Mtaa, kinachotokana na mfumo huu wa pamoja, kinaamuliwa na zoezi la tathmini ya mwaka ya utendaji ya mwaka uliopita, wakati ambapo usahihi wa matumizi ya msaada yanasimamiwa kwa karibu kwa kuzingatia matokeo katika eneo maalumu la Mamlaka ya Serikali ya Mtaa husika. Mchango muhimu wa mfumo wa LGDG umetambulika hivi karibuni hususan kwenye uimarishaji wa uwezo wa mamlaka za mitaa kwa kigezo cha utawala pamoja na usimamiaji wa mchakato wa maendeleo.

Aidha kupitia miradi mbalimbali ya kiufundi, Japan pia inasaidia katika kuimarisha uwezo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ili ziweze kutumia vizuri mfuko huu wa pamoja. Inatarajiwa kwamba kwa kuchanganya aina mbili za misaada yaani misaada ya kifedha kupitia mfuko wa pamoja na ile misaada ya ushirikiano wa kiufundi, utawala wa umma na kifedha utaboreshwa katika ngazi ya serikali za mitaa.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency