Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Shughuli katika Tanzania

Mfuko wa Pamoja wa Programu ya Marekebisho ya Serikali za Mitaa Awamu ya Pili

Aina Muda Shirika la Tanzania Gharama (Yen Mill.)
Ruzuku Julai 2009 - Juni 2012 Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 50

Katika ushirikiano wake na Tanzania, Japan ilichagua sekta za kilimo na miundombinu kama sekta za kupewa kipaumbele katika ushiriakiano huo. Hata hivyo ili mafanikio yapatikane katika sekta hizo ni muhimu kuwe na utawala bora katika ngazi za Serikali za mitaa. Umuhimu huo unaongezeka hasa kwa kipindi hiki ambapo mchakato wa upelekaji wa madaraka mikoani unaendelea kwa kasi Programu ya Marekebisho ya Serikali za Mitaa ilianzishwa mwaka 2000 kwa madhumuni ya kuweka mfumo wa upelekaji wa madaraka mikoani na uendelezaji wa uwezo wa Mamlaka za Mitaa, ambapo programu inasimamiwa kupitia usaidizi wa mfuko wa pamoja unaofadhiliwa na Serikali ya Tanzania pamoja na wabia wa maendeleo.

Awamu ya kwanza ya Programu hii ilimalizika mwezi Juni 2008, na baada ya kipindi cha mpito cha mwaka mmoja, awamu ya pili ilianzishwa katika mwaka wa fedha wa 2010. Japani ilianza kuchangia Yen milioni 50 kwa mwaka toka mwaka 2009 ili kusaidia jitihada za kupunguza umaskini zinazofanyika katika ngazi ya umma hususani katika maeneo ya vijijini.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency