Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Shughuli katika Tanzania

Mfuko wa Pamoja wa Programu ya Marekebisho ya Usimamizi wa Fedha za Umma

Aina Muda Shirika la Tanzania Gharama (Yen Mill.)
Ruzuku Julai 2008 - Juni 2010 Wizara ya Fedha 50

Kwa kuwa utawala mzuri wa huduma za umma unaweza kuathirika pale ambapo hakuna fedha usimamizi wa fedha za umma ukijumuisha mapato, bajeti, usimamiaji wa hazina, utoaji taarifa na ukaguzi wa hesabu ni eneo muhimu la utawala. Inakadiriwa kuwa asilimia 40 ya bajeti ya mwaka ya taifa ya Tanzania inafadhiliwa na wahisani. Kwa hivyo ni suala muhimu sana kwa wahisani na Serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba msaada huo unatumiwa ipasavyo. Serikali ya Tanzania ikiongozwa na Wizara ya Fedha wameendeleza Programu ya Marekebisho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP), kwa msaada unaotoka kwa wabia wa maendeleo tangu nusu ya mwisho ya miaka ya tisini.

PFMRP ilianza awamu yake ya tatu mwaka 2008 kufuatia awamu ya kwanza iliyoanza mwaka 1998 na awamu ya pili iliyoanza mwaka 2004. Katika mwaka wa fedha wa 2009/10, Japan ilitoa msaada wa fedha wa Yen milioni 50 kwenye Mfuko wa pamoja wa PFMRP kama ilivyofanya katika mwaka wa fedha wa 2008/09.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency