Japan International Cooperation Agency
Share
  • 日本語
  • English
  • Français
  • Espanol
  • Home
  • About JICA
  • News & Features
  • Countries & Regions
  • Our Work
  • Publications
  • Investor Relations

Shughuli katika Tanzania

Afya

Jitihada kubwa zimefanywa kuboresha hali ya afya nchini Tanzania. Matokeo ya jitihada hizi ni kwamba kwa miaka ya karibuni kumekuwa na kupungua kwa viwango vya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano na vya watoto wachanga. Hata hivyo, bado kuna changamoto nyingi kama vile upatikanaji finyu wa huduma za afya ya msingi uwezo mdogo wa usimamiaji wa afya katika ngazi ya wilaya, upungufu wa wafanyakazi wa afya, upungufu wa vifaa tiba na ukosefu wa miundombinu ya afya.

Kwa hiyo, kiwango cha vifo vya wajawazito bado ni kikubwa (460/100,000 LB kwa mwaka 2010). Isitoshe nchi bado ina upatikanaji mdogo wa huduma ya afya na wa maji safi.

JICA imeweka kipaumbele katika uimarishaji wa mifumo ya afya, hususani kwa kulenga kwenye mfumo wa usimamizi wa afya katika ngazi za Wilaya na Mikoa, rasilimali watu katika mifumo ya habari za afya, 5S-Kaizen katika vituo vya afya na kujenga uwezo katika kudhibiti VVU/UKIMWI

Ili kuchangia katika lengo la serikali ya Tanzania katika sekta hii, JICA inatumia uzoefu ilioupata katika miradi ya ushirikiano iliyotekelezwa hapa nchini huko nyuma.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency