Japan International Cooperation Agency
Share
  • 日本語
  • English
  • Français
  • Espanol
  • Home
  • About JICA
  • News & Features
  • Countries & Regions
  • Our Work
  • Publications
  • Investor Relations

Shughuli katika Tanzania

Usimamizi wa Rasilimali za Maji/ Majanga

Ripoti ya Wizara ya Maji ya Desemba 2009 inasema kwamba asilimia 84 ya watu wanaoishi mijini na asilimia 58.7 ya vijijini katika Tanzania Bara wanapata maji safi na salama. Ripoti hii inaonesha wazi kwamba idadi ya watu wanaopata maji salama katika maeneo ya vijijini ni ya kiwango cha chini ikilinganishwa na ile ya wanaoishi maeneo ya mijini. Hata hivyo, hali halisi inaweza kuwa ni mbaya zaidi kama tukifikiria kama kweli miundombinu ya maji inafanya kazi au la. Hali kama hiyo inatokana na matatizo mbalimbali yanayosababishwa na mambo tofauti yakiwemo masuala ya jiografia ya eneo husika, ubora wa maji, wingi wake na msimu ambao maji yanapatikana. Zaidi ya haya, uhaba mkubwa wa miundombinu ya maji, matatizo ya utunzaji wa miundombinu, na kiwango kidogo cha ufahamu wa wakazi juu ya utumiaji wa maji salama pia yanachangia hali kama hiyo.

"Dira ya 2025" ya Serikali ya Tanzania inalenga kufikisha kiwango cha upatikanaji wa maji kufikia asilimia 90 (maeneo ya vijijini) na asilimia 100 (maeneo ya mijini) ya idadi ya watu watakaopata maji salama ifikapo mwaka 2025, kuimarisha uwezo wa kusimamia rasilimali ya maji n.k. Mkakati wa Taifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini awamu ya pili (MKUKUTA2 / NSGRP2) unazingatia kuongezeka kwa kiwango cha upatikanaji wa maji kama moja ya kipaumbele muhimu katika ajenda yake. Nchini Tanzania, "Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Maji (WSDP)" unatekelezwa kwa kuzingatia "Sera ya Taifa ya Maji" na "Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Maji".

Kufuatana na Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Maji wa Serikali ya Tanzania, Japani inatia mkazo kwenye msaada wa kuboresha upatikanaji wa maji salama na safi katika maeneo ya vijijini na kuhamasisha utumiaji endelevu na unaofaa wa rasilimali finyu za maji upande wa Tanzania Bara. Kwa upande wa Zanzibar, Japani inatoa msaada wa usambazaji wa maji katika njia endelevu na ya uhakika katika maeneo ya mijini.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency