Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Shughuli katika Tanzania

Mradi wa Usambazaji wa Maji Vijijini katika Mikoa ya Mwanza na Mara

Aina Eneo Muda Shirika la Tanzania Gharama (Yen Mill.)
Ruzuku Mwanza, Mara Mei 2009 -
Desemba 2013
Wizara ya Maji 1022

picha

Kulingana na ripoti ya Wizara ya Maji ya Desemba mwaka 2007, idadi ya watu wanaopata maji safi na salama ni asilimia 58.1 katika Mkoa wa Mwanza na asilimia 48 katika Mkoa wa Mara.

Katika mradi huu, visima virefu 182 vyenye pampu za mikono na mtambo wa usambazaji wa maji unaotumia chemchem ya maji vitatengenezwa katika vijiji 26 vya Mkoa wa Mwanza (vyenye watu 2,930,000), na vijiji 18 vya Mkoa wa Mara (vyenye watu 1,360,000). Baada ya kujengwa visima hivi, inatarajiwa kwamba watu 46,000 zaidi watapata maji salama, na idadi ya watu wanaopata maji safi katika maeneo ya mradi huu itaongezeka kutoka asilimia 6 (mwaka 2005) mpaka asilimia 22 (matarajio ya mwaka 2020). Hivyo mradi huu umelenga kuboresha maisha ya wakazi wa maeneo haya.

Imepangwa kwamba usimamizi na utunzaji wa miundombinu itakayojengwa utafanywa na vikundi vya wakazi wa maeneo husika. Hata hivyo wakati mwingine inaweza kujitokeza hali ambayo hata matengenezo rahisi hayataweza kufanywa na wakazi wenyewe, au spea za matengenezo hazitaweza kununuliwa kutokana na kuchelewa kwa kulipa bili ya maji, na hali kama hiyo inaweza kuzuia kazi za miundombinu ya maji. Kwa kuzingatia hali hiyo, mradi huu utatekeleza sio tu ujenzi wa miundombinu peke yake, bali pia kwa kupitia mradi huu vyama vya watumiaji wa maji vitaanzishwa. Aidha yatatolewa mafunzo juu ya usimamizi na utunzaji wa miundombinu kwa wakazi wa maeneo husika.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency