Aina | Eneo | Muda | Shirika la Tanzania | Gharama (Yen Mill.) |
---|---|---|---|---|
Ufundi | Bonde la Wami/Ruvu | Desemba 2010- Julai 2013 |
Wizara ya Maji | 450 |
Bonde la mto Wami/Ruvu, ambalo linajumuisha miji mikubwa kama Dodoma ambao ni mji mkuu, Dar es Salaam ambao ni mji wa biashara, na Morogoro, linasambaza maji mengi zaidi katika Tanzania. Aidha kutokana na ukuaji wa uchumi unaoendelea hivi sasa, mahitaji ya maji yanatarajiwa kuongezeka.
Hata hivyo, rasilimali za maji hasa kiasi cha maji yaliyoko chini ya ardhi na mahitaji ya maji katika sekta mbalimbali kwenye bonde hili hayajajulikana wazi, na hali hiyo inaufanya usimamizi wa rasilimali za maji kutotekelezwa kama unavyotakiwa.
Katika mradi huu, katika maeneo ya bonde hili shughuli mbalimbali zinatekelezwa zikiwa ni pamoja na ufafanuzi wa mifumo ya upatikanaji wa rasilimali za maji (hasa maji yaliyoko chini ya ardhi) na utumiaji wa maji, uchoraji wa ramani ya kijiolojia ya maji, uboreshaji wa uratibu wa ukaguzi wa rasilimali za maji na kazi za uratibu wa vibali vya matumizi ya maji, na uamuzi wa mpango juu ya usimamizi wa rasilimali za maji na maedeleo kwa jumla.
Kwa ajili ya mradi huu, jumla ya watafiti 16 wanafanya kazi pamoja na wafanyakazi wa Idara ya Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji, na wengine kutoka Ofisi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu.
scroll