Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Shughuli katika Tanzania

Mradi wa Maendeleo ya Usambazaji Maji Zanzibar Mjini

Aina Eneo Muda Shirika la Tanzania Gharama (Yen Mill.)
Ruzuku Zanzibar Juni 2006- Machi 2008/
Feburari 2009- Agosti 2010
Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi 1,230/
1,419

picha

Mitambo ya usambazaji maji ilijengwa na kupanuliwa katika maeneo ya mjini Zanzibar tangu miaka ya 1920. Mitambo ya usambazaji maji sasa imezeeka, na mahitaji ya maji kulingana na ongezeko la watu yamezidi uwezo wake.

Madhumuni ya mradi huu yalikuwa ni kuwapa wakazi laki nne na sitini elfu wa Zanzibar maji salama na ya uhakika kwa kuchimba visima vipya 11. Kati ya visima hivyo, visima sita vilikamilika katika awamu ya kwanza ya mradi. Aidha wakati wa awamu hiyo, matangi ya kutunzia maji, mabomba kwa ajili ya usambazaji na pampu vilijengwa.. Kupitia awamu hii, eneo la Mji Mkongwe la Manispaa ya Zanzibar na maeneo mengine ya jirani yalipata maji safi na salama. Katika awamu ya II, visima vitano zaidi vilichimbwa pamoja na kujengwa matangi mawili zaidi ya kuhifadhia maji kwa ajili ya usambazaji

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency