Japan International Cooperation Agency
Share
  • 日本語
  • English
  • Français
  • Espanol
  • Home
  • About JICA
  • News & Features
  • Countries & Regions
  • Our Work
  • Publications
  • Investor Relations

Shughuli katika Tanzania

Uimarishaji wa Usimamizi wa Usambazaji wa Maji katika Mamlaka ya Maji Zanzibar

Aina Eneo Muda Shirika la Tanzania Gharama (Yen Mill.)
Ufundi Zanzibar Septemba 2007 -
Desemba 2010
Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi 280

picha

Tangu Zanzibar iwe huru mwaka 1963, mitambo yote ya maji ya Zanzibar ilisimamiwa na kutunzwa na Serikali ya Zanzibar, ambayo pia ilitoa maji ya bure kwa wananchi wake. Kwa bahati mbaya, hali mbaya ya kifedha imeizuia serikali kukarabati mitambo ya maji iliyozeeka na pia kutengeneza rasilimali mpya za maji, hivyo kuwanyima watu wengi maji salama na ya uhakika.

Chini ya Mradi wa Maendeleo ya Usambazaji Maji Zanzibar Mjini, Japani ilitoa msaada wa kutengeneza vyanzo vipya vya maji na kuboresha mifumo ya usambazaji maji, lakini jitihada nyingine endelevu zilihitajika kwa madhumuni ya kuimarisha upatikanaji wa maji salama. Ili kufanya hivyo ulipiaji sahihi wa huduma ya maji na ukusanyaji wa mapato yatokanayo na huduma hiyo lazima vifanyike ili kuitunza na kuikarabati mitambo ya usambazaji maji. Hivyo, mradi huu ulishinikiza kuanzishwa kwa mfumo wa ukusanyaji wa mapato yatokanayo na huduma ya maji chini ya Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA). Mfumo huu ulianzishwa mwaka 2006.

Chini ya mradi huu, JICA ilileta wataalamu watano ZAWA ili kutoa mafunzo kwa uongozi wa Mamlaka katika maeneo yanayohusika kama maandalizi ya kuweka kumbukumbu za wateja, ukusanyaji mapato na huduma kwa wateja.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency