Japan International Cooperation Agency
Share
  • 日本語
  • English
  • Français
  • Espanol
  • Home
  • About JICA
  • News & Features
  • Countries & Regions
  • Our Work
  • Publications
  • Investor Relations

Tovuti Maalum ya Maadhimisho ya Miaka 60

MIAKA 60 YA USHIRIKIANO WA JICA NA TANZANIA

JICA iliadhimisha miaka 60 ya ushirikiano wake na Tanzania mwaka 2022. Shughuli za ushirikiano huo zilianza mwaka 1962, mwaka mmoja tu baada ya uhuru wa Tanganyika, baada afisa mmoja wa Serikali kukubaliwa kupata mafunzo ya kiufundi nchini Japani.

Tangu wakati huo, shughuli za JICA ziliendelea kukua, na sasa ushirikiano huo sio tu wa mafunzo ya kiufundi na uletaji wa na wataalamu wa Kijapani wa kujitolea (JOCV), lakini pia utoaji wa misaada na mikopo yenye masharti nafuu.

Hadi Agosti 2022, Tanzania ilikuwa imepokea mikopo yamasharti nafuu yenye thamani ya zaidi ya Dola Bilioni 1.0, Dola Bilioni 1.2 za Msaada isiyokua na sharti la kulipa, na Dola Bilioni 0.9 za Ushirikiano wa kiufundi. Katika kipindi hicho, JICA imetoa fursa za mafunzo kwa Watanzania 22,064 nchini Japani, katika nchi nyingine na ndani ya Tanzania na kutuma Wajapani wa kujitolea 1, 679 katika nyanja mbalimbali.

Photo


[Assistance To Tanzania From JICA]
ODA Loan: 115.4 Billion Japanese Yen
Training Program: 22,064 Participants, *The number includes participants of JICA Training in Japan, Third Country Training Program, and In-country Training Program
Technical Cooperation: 97.3 Billion Japanese Yen
JOCV: 1,679 Volunteers
Grant Aid: 131.5 Billion Japanese Yen
1USD=106.9JPY(Based on the past 10 years average exchange rate)

JICA husaidia mipango ambayo Watanzania kwa jitihada zao hujiwekea kwa ajili ya kujiletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi sambamba na dira yake ya "Kuongoza ulimwengu kwa uaminifu". Shughuli za JICA Tanzania pia zinarandana na maazimio ya Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo juu ya Mchakato wa Maendeleo ya Afrika (TICAD) ambao huipa nafasi Afrika ya kujiongoza na Ushirikiano Kimataifa - mchakato ambao ulianza mnamo 1993.

Ushirikiano wa JICA kwa Tanzania umekuwa ukitekelezwa kulingana na Mipango na Vipaumbele vya Maendeleo ya Tanzania.

Photo


  • Katika kipindi cha miaka 60, shughuli za JICA zimeendelea kukua na kupanuka ili kusaidia maendeleo ya shughuli za kijamii na kiuchumi.
  • Ushirikiano wa JICA unategemea vipaumbele vya Tanzania. Hivyo, JICA itaendelea kutekeleza shughuli zake kulingana na mipango ya maendeleo ya Tanzania.

Photo


Kwa maelezo zaidi fungua link hii:

[Video] MIAKA 60 YA USHIRIKIANO WA JICA NA TANZANIA

Photo

Photo


Kwa maelezo ya kina tembelea ukurasa wetu wa Facebook:

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency