Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Taarifa kwa Umma

11 Oktoba 2021

Kwa ajili ya usalama wa Watanzana - sekta ya matengenezo ya magari nchini Tanzania yaungwa mkono na Wajapani wa waliopita kujitolea wa JICA

Aliyekuwa Mjapani wa kujitolea kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani (JICA), Bwana MUROYA Koji ambaye hapo awali alikua anafanya kazi VETA Mwanza kuanzia 2013 hadi 2015 kama mtaalamu wa ufundi wa magari, amerudi tena Tanzania na sasa anafanya kazi katika Kampuni ya Saint Parts Ltd iliyopo Dar es Saoaam.

Bwana MuUROYA ni mmoja kati ya Wajapani 143 ambao waliletwa nchini chini ya program ya Wajapani wa kujitolea wa JICA (Japan Overseas Cooperation Volunteers - JOCV) katika sekta ya uhandisi wa magari.

Alipoulizwa ni kitu gani kilimsukuma hata akaamua kurudi Tanzania, alitaja sababu nyingi lakini alitaja chache zilizochomoza kama hizi: ‘uzoefu mzuri alioupata nchini wakati alipokua anafanya kazi ya kujitolea, uelewa wa tamaduni za Tanzania ikiwepo lugha ya Kiswahili n.k. Alidai vitu hivi vyote vilimfanya arudi Tanzania, nchi aliyodai anaipenda sana. Aidha kwa kuongezea, alisema kuwa ikilinganishwa na Japan, ambapo watu kwa kawaida wana shughuli nyingi na watulivu, Watanzania ni marafiki sana na jinsi wanavyosalimiana kila wanapokutana ilimvutia sana"

Akielezea shughuli za Kampuni yake ambapo kwa sasa ni Meneja wa Tawi la Tanzania, anasema kwa kujigamba kuwa kampuni hiyo inashughulika na shughuli nyingi ikiwa ni pamoja na uingizaji wa magari na usambazaji wa vipuri halisi vya magari ya kijapan, matairi, mafuta ya magari nk. Anasema kuwa kampuni hiyo inatoa huduma zenye ubora wa hali ya juu ambazo zimekubaliwa vizuri na wateja na kulingana na mafanikio hayo, kampuni yake inakusudia kupanua huduma zake ili kufikia wateja zaidi nchini na hata kufikia nchi jirani.

Juu ya usiri wa kuendesha magari kwa usalama, alitoa ushauri huu kwa madereva wote: ‘Matengenezo ya magari ya mara kwa mara na ukaguzi wa magari ikiwa ni pamoja na matairi ni mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa magari kwa usalama".

Aidha aliongeza kusema kuwa, kampuni yake ilijiunga na utafiti wa JICA wa kukuza sekta ya ufundi wa magari wa viwanda mwaka 2019. Utafiti huo ulilenga kutambua masuala ya utunzaji rasimali watu na mbinu za hali ya juu za matengenezo na mfumo wa uthibitisho wa gereji za matengenezo pamoja na ukaguzi wa usalama wa magari nchini.

PhotoMr. Muroya akiwa kwenye garage yake DSM


Kuhusu Program ya Wataalam wa Kujitolea kutoka Japani (JOCV)

JOCV ni programu chini ya Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani (JICA). JOCV ilianzisha shughuli zake nchini Tanzania mnamo 1965 na kufikia Machi 2020, zaidi ya wajapani wa kujitolea 1,700 walikuwa wametumwa kufanya kazi katika sekta na maeneo mbalimbali ya Tanzania. Programu hii ina madhumuni ya kusaidia nchi zinazoendelea kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kusisitiza kujitegemea kwa mabadiliko endelevu katika sekta mbali mbali.

Kuhusu Saint Parts Co, Ltd.

Kampuni hii ilianzishwa mwaka 2013 huko Japani, kama chombo cha kutengeneza magari chenye jukumu kubwa katika utunzaji wa mazingira. Kampuni hiyo ilianzisha tawi lake la kwanza nchini Tanzania mnamo mwaka 2018 na ilifungua karakana ya kisasa ya kukarabati na matengenezo ya magari ya Japani. Huduma zingine ni pamoja na: uuzaji wa vipuri vya hali ya juu vilivyotumika na vipya, matairi ya Yokohama, mafuta ya Takumi, uingizaji wa magari kulingana na ombi la mteja, n.k. Kampuni inajitahidi kuendelea kutoa huduma bora na kwa gharama nzuri kwa wateja wake nchini Tanzania na nchi jirani.

Website: https://japancar.co.tz (external link)
Contact in Tanzania: tanzania@saintparts.co.jp
OFFICE: +255 657 109 001

Utafiti wa Uundaji wa Biashara ya SDGs na Sekta Binafsi ya Kukuza Mitambo ya Gari na Mtandao wa Viwanda cha Matengenezo ya Magari kupitia Matengenezo ya Gari katika Mazoezi ya Kitaalam nchini Tanzania SAINT PARTS Co, Ltd. (Hashima-City, Gifu Pref., Japan)

Hii ni moja ya tafiti zilizofanywa chini ya mpango wa JICA kwa uhusiano na sekta binafsi. Utafiti huo ulianza mnamo 2019 na umefanywa ili kujenga mifumo na miundombinu ya kutekeleza miradi ya mafunzo ya majaribio ya ufundi wa utunzaji wa gari zinazotolewa na VETA kupitia mtaala wa mafunzo na vifaa kwa kutumia karakana yetu nchini Tanzania na mitambo ya Kijapani: Washiriki katika utafiti huo ni: Mamlaka ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi (VETA), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Chuo cha Ufundi cha Arusha (ATC), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (MWTC).

Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na:
JICA Tanzania Office, P.O. Box 9450,
Dar es Salaam, Tel: 022-211327/30
Ms. Reiko.Abo. jicatz-vcs@jica.go.jp
Ms. Catherine Shirima: ShirimaCatherine.Tz@jica.go.jp

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency