Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Taarifa kwa Umma

06 Novemba 2021

Utafiti wa Uboreshaji wa Usafiri wa Reli za Abiria Mijini Kuanza jijini Dar

Dar es Salaam. Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani (JICA), Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Shirika la Reli Tanzania (TRC) wamekubaliana kutekeleza mradi wa utafiti wa ukusanyaji wa data na uboreshaji wa usafiri wa reli za abiria jijini Dar es Salaam kuanzia mwezi huu.

Kwa mujibu wa mkutano wao wa kwanza uliofanyika Novemba 4, 2021 jijini Dar es Salaam, utafiti huo wa miezi minne unaotarajia kukamilika Februari 2022, utachunguza miundombinu ya reli za abiria zilizopo Dar es Salaam (reli ya Pugu na Ubungo) na kupendekeza hatua mbalimbali za kuboresha miundombinu hiyo.

Mkutano huo uliohudhuriwa na washiriki 18 kutoka Ofisi ya JICA Tanzania, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, TRC na Washauri kutoka Japani na Tanzania walipendekeza mpango wa uboreshaji wa ufuatiliaji wa uendeshaji wa reli, uwekaji ishara, usafirishaji wa bidhaa, ujenzi wa stesheni katika vituo, majengo ya biashara katika stesheni na namna bora ya kutoa huduma ya usafiri katika njia za treni za abiria zilizopo.

Timu ya watafiti iliyoundwa, itajadiliana na maafisa wa serikali ya Tanzania ili kurekebisha Mpango Kabambe wa Usafiri wa Mijini wa Dar es Salaam wa mwaka 2018, ambao ulifadhiliwa na JICA.

Mpango huo kabambe unakadiria kwamba Dar es Salaam itakuwa na zaidi ya watu milioni 10 mapema mwaka 2030, hivyo usafiri wa barabara pekee hautaweza kutoa usafiri wa uhakika na kuondoa kero ya msongamano wa magari (foleni) na kutumia muda mrefu wa kusafiri ndani ya jiji hilo.

Mkutano huo pia ulipendekeza namna bora ya uboreshaji wa mfumo wa reli uliopo kwa ajili ya maendeleo ya usafiri na mipangilio mizuri yenye uwiano.

Mikutano zaidi ya majadiliano itaendelea kufanyika kila inapohitajika, hadi kukamilika kwa utafiti huo mnamo Februari 2022.

Shirika la la Maendeleo la Kimaitaifa la Japani (JICA) limekuwa likisaidia sekta ya uchukuzi kwa zaidi ya miaka 40 hapa Tanzania.

Kwa habari zaidi, tafadhali wasiliana na:
Bw.. Henry R. Kajange
JICA Tanzania Office
Tel: +255-787-464-620
E-mail: Kajange-Henry@jica.go.jp

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency