Japan International Cooperation Agency
Share
  • 日本語
  • English
  • Français
  • Espanol
  • Home
  • About JICA
  • News & Features
  • Countries & Regions
  • Our Work
  • Publications
  • Investor Relations

Taarifa kwa Umma

13 Aprili 2022

JICA kuifanya Dar es Salaam kuwa sehemu nzuri ya kuishi, endelevu na bora

Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) limekuwa likisaidia sekta ya usafirishaji nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 40. JICA na Serikali ya Tanzania wamesaini Mkataba wa Majadiliano (RD) wa Mradi wa Ushirikiano unaoitwa "Transit-Oriented Development (TOD), Dar es Salaam".

TOD, ambayo itatekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na JICA kwa mara ya kwanza katika safari ya maendeleo ya kiuchumi ya nchi, ni njia ya kupanga (mapema) na kuandaa maendeleo ya mijini kwa ubora na urahisi katika miundombinu na huduma za usafiri wa umma. Ni moja ya mikakati madhubuti ya kuondoa msongamano wa magari Dar es Salaam kama ilivyopendekezwa katika Mpango wa Usafiri wa Dar es Salaam uliofadhiliwa na JICA mwaka 2018.

Kutokana na maombi kutoka Serikali ya Tanzania, JICA ilileta timu ya wataalamu Tanzania tarehe 3 Februari, 2022 hadi Februari 8, 2022 kwa ajili ya mradi wa TOD kwa Dar es Salaam.

Timu hiyo ilifanya majadiliano na Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wakala wa Usafiri wa Haraka (DART), na wadau wengine kuandaa mpango wa kina wa mradi huo.

Lengo la mradi kwa ujumla ni kuhamasisha matumizi ya TOD katika mipango ya mji wa Dar es Salaam na kusudi la mradi ni kuongeza uwezo wa taasisi husika kutumia njia ya TOD kwa mipango ya miji, na kuboresha utumiaji wa mabasi yaendayo haraka (BRT) na kuanzisha utaratibu wa uratibu wa mipango na utekelezaji.

Muda wa Mradi ni miezi 36 kutoka Juni 2022 hadi Mei 2025.

Dhana ya mradi unahusisha kubadilishana utaalamu na kujenga uwezo wa aina mbalimbali kama vile ushirikiano katika kufanya kazi, mafunzo ndani ya kazi, na semina kuhusiana na mpango wa maafisa wa wadau wanaohusika.

Uunganishwaji na njia nyingine za usafiri katika vituo vingine zitaboreshwa. Mtandao wa mabasi yanayoleta abiria kwenye vituo vya BRT (ramani za njia, vituo vya basi, masafa, wakati wa kufanya kazi, na nauli) zitajumuishwa.

Pi, mradi unatarajia kuboresha vituo vya BRT viweze kufikiwa kwa usalama, raha na kwa ufanisi. Vituo vitaundwa kwa mfumo rafiki kwa mtumiaji.

Aidha, mradi utatoa Miongozo na Mikakati ya TOD kama nyaraka zitazoongoza, majukumu na wajibu wa taasisi, mchakato wa upangaji na utekelezaji wa TOD na kuonyesha muundo wa miji, vituo, na nodi kwenye mitandao ya usafiri katika barabara zote za BRT jijini Dar es Salaam.

Baadae, ambapo Miongozo na Mikakati itazingatiwa na kutekelezwa na wadau, Mradi wa TOD utaongoza jiji la Dar es Salaam katika maendeleo yake endelevu. Bila shaka jiji hilo litakuwa la kuvutia kwa maisha ya watu, na kuwa lango la kiuchumi katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati. Mradi utachangamsha shughuli za kiuchumi na ufanisi, jamii yenye fursa sawa kwa wote, maisha bora na salama na mazingira ya kuvutia.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Mr. Henry R. Kajange
JICA Tanzania Office
Tel: +255-787-464-620
E-mail: Kajange-Henry@jica.go.jp

PhotoTOD kwenye BRT, Bogota, Colombia (Taarifa ya WB)

PhotoStesheni ya Tokyo (Katikati ya Mji), Japan (JICA)

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency