Japan International Cooperation Agency
Share
 • 日本語
 • English
 • Français
 • Espanol
 • Home
 • About JICA
 • News & Features
 • Countries & Regions
 • Our Work
 • Publications
 • Investor Relations

Taarifa kwa Umma

15 Juni 2022

Kampuni ya Fumakilla Kutoka Japani Imetembelea Tanzania Kufanya tathmini ya mahitaji ya bidhaa kuzuia mbu wa malaria na Dengu.

Kampuni ya Kijapani, Fumakilla Limited, ambayo imekuwa ikitengeneza viuadudu vya nyumbani kwa zaidi ya miaka 100, inapanga kuanzisha teknolojia ya hali ya juu ya kupambana na mbu ili kupambana na malaria, homa ya "dengue" na magonjwa mengine ya kuambukiza yanayohusiana na mbu nchini kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani (JICA).

Kwa teknolojia hiyo, bidhaa hiyo mpya (koili ya mbu) hutoa moshi kidogo wa kuua mbu inapotumika ndani ya nyumba na inafukuza mbu inapotumiwa nje.

"Koili mpya ya mbu ni bidhaa yenye ufanisi mkubwa dhidi ya mbu wa kienyeji. Wakati huo huo, imepata kiwango cha juu cha usalama ambacho kimeainishwa kama Daraja la U (haiwezi kuleta madhara makubwa) na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO). Ni uainishaji wenye moshi kidogo sana. Zaidi ya hayo, bei yake itakuwa nafuu kwa watu wengi," alisema Bw. Toshiaki Muramoto, mkuu wa ujumbe wa Fumakilla Limited uliotembelea Tanzania katikati ya mwezi Mei 2022 kwa ajili ya tathmini ya mahitaji inayoungwa mkono na JICA.

Katika ziara hiyo, wajumbe hao walitembelea maeneo ambayo yameathirika zaidi na malaria na "dengue". Ziara yao ilikuwa ya kwanza tangu kuidhinishwa kwa mradi wa Fumakilla kama Mpango wa Ushirikiano wa Kibinafsi wa JICA mwaka wa 2019, kutokana na vikwazo vikali vya usafiri vilivyowekwa Japani kutokana na ugonjwa wa UVIKO-19.

Hatua hiyo imekuja baada ya Bw.Toshiaki Muramoto, Mjapani aliyefanya utafiti wa mfumo wa kilimo katika Mkoa wa Morogoro nchini Tanzania kwa takriban mwaka mmoja, miaka 27 iliyopita, kwa msaada wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.

Nilipokuwa kijijini, nilitembelea mashamba kila siku kuwahoji wakulima na kukusanya udongo kwa ajili ya majaribio ya kimaabara. Nikiwa nafanya kazi shambani niliumwa na mbu na nikaugua malaria mara tatu ndani ya mwaka mmoja na kulazwa hospitalini mara mbili," alibainisha.

Baada ya kumaliza masomo yake, alirudi Japani na kuamua kufanya kazi katika kampuni ya Fumakilla Limited, na aliona kuna haja ya kuitambulisha koili iliyotengenezwa kwa tekinolojia ya hali ya juu inayoua mbu, kama bidhaa muhimu katika kudhibiti malaria nchini Tanzania.

Bidhaa ya Fumakilla tayari imefanyiwa majaribio na kuidhinishwa na Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kitropiki (TPRI), wakala wa serikali ambao wanadhibiti matumizi ya viua wadudu nchini Tanzania.

Utafiti wa tathmini ya mahitaji ya Fumakilla, ukiungwa mkono na JICA, ulianza Oktoba 2020 na utakamilika mwaka 2023, kwa ziara tatu zaidi zilizopangwa nchini Tanzania.

Wakati wa ziara yao, ujumbe ulifanya mijadala ya vikundi na jumuiya za wenyeji ili kuangalia utangamano wa ndani wa bidhaa za Fumakilla. Aidha ilitoa bidhaa hizo kwa wakazi kwa ajili ya majaribio ya matumizi ya nyumbani na kufanya warsha kwa ajili ya kuongeza uelewa wa umma.

Maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya utafiti huo ni Mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Pwani, Mwanza na Mtwara.

Katika ziara hii ya kwanza ya JICA-Fumakilla ya tathmini, timu ilifanya vikao vya mashauriano na maafisa wa serikali wanaosimamia udhibiti wa vijidudu vya magonjwa katika Wizara ya Afya (MoH) na Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-AMISEMI) kuhusu uwezekano wa kutumia bidhaa ya Fumakilla kama njia ya kudhibiti vekta na uwezekano wa ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi kwa ajili ya kuendeleza uzuiaji wa malaria.

Photo

Photo


For more information please contact:
Ms. Flavia Manyanga
JICA Tanzania Office, P.O. Box 9450, Dar es Salaam
Tel: 022-211327/30 Fax: 022-2112976 Mobile: 0789-854615
Email: Manyangaflavia.TZ@jica.go.jp

PAGE TOP