Japan International Cooperation Agency
Share
  • 日本語
  • English
  • Français
  • Espanol
  • Home
  • About JICA
  • News & Features
  • Countries & Regions
  • Our Work
  • Publications
  • Investor Relations

Taarifa kwa Umma

09 Novemba 2022

MAZINGIRA YA TANZANIA YAMVUTIA MTAALAM WA JICA WA KUJITOLEA KUHAMASISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Mjapani mmoja aitwaye Bi. Ayusa OKUI, ametayarisha vitabu viwili vya sinema viitwavyo "Kijiji wa Tup Tupa na "Hazina ya Bibi na Babu", na kuviingiza kwenye mtandao wa YouTube kwa lengo la kuhimiza utunzanji wa mazingira nchini Tanzania.

"Sababu kubwa ya kutayarisha vitabu hivi ni kwa upendo nílio não kwa Tanzania, watu wake na mazingira yake. Natumaini mazingira haya yataendelea kama yalivyo".

Bi. OKUI alikua ni mtaalam wa kujitolea kupitia Mpango wa Wataalam wa Kujitolea wa Japan uitwao (JOCV), ambao ni mojawapo wa mipango ya Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani (JICA).

Alifanya kazi kama Ofisa wa Maendeleo ya Jamii katika Kata ya Ifunda, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuanzia mwaka 2017 - 2020. Katika muda huo wa miaka miwili alipata fursa ya kutembelea vijiji kadhaa. Alifanya hivyo kwa kutembea kwa miguu au kutumia baiskeli. Katika matembezi yake hayo alivutiwa sana na misitu aliyoiona na hali hiyo ilimfurahisha.

Hata hivyo alistuka alipoona miti mizuri ilpokua inakatwa ovyo na hivyo kupelekea hifadhi ya misitu kupotea kila uchao. Ingawaje alielewa kua miti hutumika katika shughuli mbalimbali kama vile kupikia na mambo mengine, hali hiyo ilimfanya aanze kufikiria njia mbadala za kuweza kutumiwa na watu kuhifadhi rasilmali za maliasili.

Kutokana na hayo alianza kubuni hadithi mbalimbali zinazohusu uhifadhi wa mazingira zikiwa zimeboreshwa kwa kuwekewa picha za sinema na kuziweka katika mtandao wa YouTube. Ana imani kwamba hadithi hizo zitachochea watu kuhifadhi mazingira, hatua ambayo itaifanya jumuiya ya Watanzania kuwa na maisha bora.

Haikuwa kazi rahisi kutengeneza "video" hizo lakini tayari ameshatengeneza video kadhaa za namna hiyo na kuziingiza mtandao wa YouTube.

Bi. OKUI anasema kwamba inamchukua kama miezi miwili hivi kutayarisha hadithi na "video" moja. Aidha anasema yeyé binafsi hufanya kazi zote za kutengeneza "video" husika yaani, kubuni hadithi, kuchora picha, kutafsiri hadithi hizo kua za lugha ya Kiswahili, kurekodi na hatimaye kuhariri video hizo. Hata hivyo anasema kwamba kuna Mwalimu mmoja Mtanzania anayefundisha Kiswahili ambaye yuko Japani ndiye anamsaidia kuboresha tafsiri zake.

Kwa sasa ana matumaini kwamba "video" zake zitawafanya watu wengi wafurahi na kutabasamu. Hata hivyo pamoja na yote hayo lengo lake kuu ni kuona watu wanaishi vizuri na kuwa marafiki wa mazingira.

YouTube video link: (Stories, Pictures and Narration made by Ms. OKUI above)

Kuhusu Mpango wa Wataalam wa Kujitolea kutoka Japani (JOCV):

JOCV ni programu chini ya Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani (JICA). JOCV ilianza shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1967 na kufikia Machi 2020, zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea wa Japani 1,700 walikuwa wametumwa kufanya kazi katika sekta na maeneo mbalimbali ya Tanzania. Mpango huo unalenga kusaidia nchi zinazoendelea kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kusisitiza kujitegemea kwa mabadiliko endelevu katika sekta mbalimbali

About JICA (Japan International Cooperation Agency):

JICA is an incorporated administrative agency in charge of administering Japan's ODA (Official Development Assistance). It is one of the world's largest bilateral aid agency supporting socio-economic development in developing countries in different regions of the world.

In Tanzania, JICA has been a long partner for 60 years in various sectors since 1962.

For further information, please contact:
JICA Tanzania Office, P.O. Box 9450, Dar es Salaam,
Tel: 022-211327/30 Fax: 022-2112976
jicatz-vcs@jica.go.jp

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency