Japan International Cooperation Agency
Share
  • 日本語
  • English
  • Français
  • Espanol
  • Home
  • About JICA
  • News & Features
  • Countries & Regions
  • Our Work
  • Publications
  • Investor Relations

Taarifa kwa Umma

09 Septemba 2020

"Anzia Sokoni Malizia Shambani Kwa Kipato Zaidi"
KAULI MBIU YA MRADI WA JICA WA TANSHEP

Hivi ndivyo mkulima bora huweka akilini kila wakati

"Wakulima wanapaswa kwanza kuanza kulisoma soko kabla ya uzalishaji, kwa sababu katika soko, watajua aina za mazao maarufu, ubora na kiwango cha biashara, washindani na msimu wenye bei ya juu. Nilikuwa nikilima bila kujua gharama halisi ya uzalishaji kwa sababu sikuweka kumbukumbu za shughuli za kilimo, lakini kupitia mradi huu nimeweza kujua gharama za shughuli za kilimo ikiwa ni pamoja na hesabu ya faida na hasara"- Bwana Joel Jackson Ikera, kutoka katika Kikundi cha Umoja cha Wakulima, Wilaya ya Lushoto, Mkoa wa Tanga.

Bwana Joel Ikera aliongeza uzalishaji wake kupitia maarifa ya mbinu ya SHEP aliyopata kutoka katika mradi wa TANSHEP unaodhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani (JICA). Kwa mfano, kupitia maarifa hayo aliweza kuongeza uzalishaji wa mazao tofauti tofauti kwa kila shamba (0.125 ekari) kama ifuatavyo:

  • "zukini" - kutoka kilo 320 hadi kilo 940 (karibu mara tatu)
  • "brokoli" - kutoka kilo 210 hadi kilo 520 (karibu mara mbili na nusu)
  • "kolifulawa" - kutoka kilo 420 hadi kilo 900 (zaidi ya mara mbili)

Mbali na kufanikiwa kupata ongezeko kubwa la uzalishaji kama ilivyoelezwa hapo juu, Bwana Joel Ikera ameweza kutumia vizuri ustadi wa usimamizi wa mashamba, uuzaji wa mazao na utunzaji wa kumbukumbu nk. - faida ambazo alizipata kutoka katika mradi wa JICA uliotajwa hapo juu. Hizi ndizo sababu kuu zilizomfanya achaguliwe kama "Mkulima Bora wa Kanda katika Kanda ya Mashariki ya Tanzania" katika hafla ya Sherehe za Nane - Nane za mwaka huu.

Bwana Ikera bila shaka ni mmoja wa wale wakulima ambao wanajifunza haraka jinsi ya kubadilisha fikra zao za kilimo cha kawaida kutoka "Kulima na Kuuza" na kuwa "Kulima kwa ajili ya Kuuza" kupitia miradi wa ushirikiano wa kiufundi wa JICA (TANSHEP), ambayo ni, "Mradi wa Kuimarisha Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADPs) na ule wa Upangaji na Uwezo wa Utekelezaji kupitia Matumizi ya Njia ya Uwezeshaji na Uhamasishaji kwa Wakulima Wadogo wa mazao ya bustani" (SHEP).

TANSHEP ni mradi wa miaka mitano ambao ulianza Januari 2019 na unatekelezwa na Wizara ya Kilimo na Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la

Kimataifa la Japani (JICA). Mradi ulianza na wilaya sita zilizolengwa katika mikoa mitatu ya kaskazini (Kilimanjaro, Arusha, na Tanga) huku ikilenga kuusambaza nchi nzima hatua kwa hatua.

TANSHEP inazingatia kukuza maendeleo ya kilimo cha bustani kwa kutumia "SHEP" (Uwezeshaji na Ukuzaji wa Wakulima Wadogo Wadogo wa Mazao ya Bustani) iliyoanzishwa na JICA, ambayo inatambua "Kilimo kinacholenga Soko". Njia hii inahimiza wazalishaji wa bustani kufanya uchunguzi wa soko kwanza kabla ya kushiriki katika uzalishaji. Zaidi ya hayo, njia hiyo inahimiza ushirikiano na wadau husika, kama wanunuzi, wasambazaji wa pembejeo, na hata mawakala, ili kuboresha uzalishaji na uuzaji na hivyo kuongeza mapato kwa kuboresha maisha ya vijijini nchini Tanzania.

Wakulima wa mazao ya bustani katika wilaya zilizolengwa wanatumia kwa bidii njia ya SHEP kulingana na masomo na ujasiri uliopatikana kupitia Awamu ya Kwanza ya Majaribio chini ya TANSHEP. Kuanzia mwezi huu (Septemba 2020), Awamu ya Pili ya matumizi ya njia ya SHEP itaanza. Kufuatia mafunzo kwa maafisa ugani, vikundi vya wakulima vilivyochaguliwa vitafanya ziara za mashambani kwa vikundi vya wakulima waliofanikiwa ili kujifunza mazoea mazuri (good practices) ambayo yalitokana na mabadiliko ya mawazo ya "Kulima kwa ajili ya Kuuza".

Mfululizo wa shughuli za mradi (yaani Utafiti wa awali, Utafiti wa Soko, na Uunganishaji wa wadau na wakulima) umefikia wakulima wengi (kama vikundi vya wakulima 56) na maafisa ugani katika mikoa mitatu iliyolengwa.

Kupitia shughuli hizo, mawazo ya wakulima yanaonekana kubadilika kutoka kwa mawazo ya "Kulima na Kuuza" kuwa mawazo ya "Kulima kwa ajili ya Kuuza"

kama inavyothibitishwa na uzoefu wa Bwana Joel Ikera hapo juu.

Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na:
Ofisi ya JICA Tanzania, S.L.P 9450, Dar es Salaam,
Simu: 022-211327/30 Nukushi: 022-2112976
Bi. YAMADA Namiko / 0682215969 / Yamada.Namiko@jica.go.jp
Bi. Veronica Balua / 0682216 080 / BaluaVeronica.TZ@jica.go.jp

PhotoBwana Joel Jackson Ikera, mwanachama wa Kikundi cha Wakulima cha Umoja A, Wilaya ya Lushoto. Alitunukiwa kama "Mkulima Bora wa Mwaka wa Kanda katika Ukanda wa Mashariki mwa Tanzania" katika hafla ya Sherehe za Nane Nane za miaka huu.

PhotoKupanga utafiti wa soko huko Lushoto: Kabla ya kwenda sokoni, kikundi cha wakulima kitaamua ni habari gani ya mazao wanayokusanya. Kulingana na upangaji, wakati mwingine wawakilishi wa kikundi cha wakulima hupeleka sampuli ya bidhaa zao kwenye soko la kukuza mauzo.

PhotoUtafiti wa Soko huko Arusha: Kuangalia mahitaji ya kina ya kile wauzaji wa jumla wanataka kama aina, ubora, wingi, bei ya wakati wa msimu wa juu na kadhalika.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency