Japan International Cooperation Agency
Share
  • 日本語
  • English
  • Français
  • Espanol
  • Home
  • About JICA
  • News & Features
  • Countries & Regions
  • Our Work
  • Publications
  • Investor Relations

Taarifa kwa Umma

06 Septemba 2021

Utamaduni mzuri na ukarimu wa Watanzania wawafanya Wajapani wa wajitolea kurudi kusaidia wakulima

Wajapani watatu wa kutoka Shirika la Wataalam wa Kujitolea kutoka Japani (JOCV), ambao walikuwa wanafanya kazi nchini Tanzania wameunda kampuni inayoitwa WATATU Ltd., yenye madhumuni ya kuboresha uzalishaji wa kilimo wa mkulima mmoja mmoja nchini. Kampuni hiyo ilianzishwa Desemba 2020, na tayari imewekeza Shilingi za Kitanzania milioni 40 na inafanya kazi na wakulima wa Songea, Kilombero na Njombe kama washirika wa biashara kupitia utoaji wa vifaa vya kilimo, kuwajengea uwezo, na utafiti wa masoko kwa mazao ya wakulima. Kampuni hiyo inakusudia kuinua tija ya mazao ya wakulima na baadaye kugawana faida kwa kila mmoja kwa uwiano sawa. Katika mwaka wa pili wa biashara yao, Wajapan hao wamepanga kupanua shughuli zao katika mikoa mingine.

Walipoulizwa kwa nini walihamasishwa kurudi Tanzania, Wajapani hao walisema kuwa ukarimu wa Tanzania kama sababu kuu ya uamuzi wao wa kurudi. Walisema, ukarimu ambao walipokea kutoka kwa Watanzania ulikuwa mzuri sana zaidi ya maelezo. Kwa msingi huo walidhani walikuwa na deni la kulipa kwa watu wa Tanzania, hivyo kuamua kuunda kampuni ya kushirikiana na Watanzania.

Bwana OKAMOTO, Afisa Mtendaji Mkuu wa WATATU Ltd., alisema hivi: "Tanzania imejaliwa ardhi yenye rutuba na hali ya hewa nzuri; tutatumia fursa hizi kuinua maisha ya wakulima wa Tanzania".

Hivi sasa wakulima 15 wamenufaika na ushirikiano na kampuni hii na baadhi yao walikuwa na haya ya kusema: "Ninashukuru msaada kwa sababu nimelima hekta 6 na ninatarajia mavuno mazuri tofauti na zamani ambapo nililima hekta 3 tu na kupata mavuno duni". Mkulima mwingine alisema: "Nimepata ujuzi wa kilimo na ujuzi wa uuzaji, kwa hivyo msimu ujao nimepanga kulima hekta nyingi zaidi". Aidha wengine walisema hivi: "Sikuweza kupata mkopo wa benki, lakini sasa naweza kupata na kulima vizuri "," Wakati ninahitaji vifaa, navipata kwa wakati muafaka" nk.

Kutokana na juhudi za Wajapani hao ambao zimetajwa hapo juu, pamoja na kujitolea kwao na kuwa na uzoefu na Watanzania, JICA imeamua kushirikiana na Kampuni ya WATATU kufanya Utafiti wa Kukuza Biashara ya Ufugaji Nyuki nchini Tanzania. 

Kuhusu Shirika la Wataalam wa Kujitolea kutoka Japani (JOCV)

JOCV ni Shirika ambalo liko chani ya Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani (JICA). JOCV ilianza shughuli zake nchini Tanzania mnamo 1965 na kufikia Machi 2021, zaidi ya Wajapani wa kujitolea wa Kijapani 1,700 walikuwa wametumwa kufanya kazi katika sekta na maeneo mbalimbali ya Tanzania. Shirika hili linakusudia kusaidia nchi zinazoendelea kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kusisitiza kujitegemea kwa mabadiliko endelevu. Wajapani wa kujitolea hutumwa nchini kufanya kazi katika nyanja tofauti za kitaalam kama vile kilimo, maendeleo ya jamii, elimu, afya, tasnia ya teknologia, mafunzo ya ufundi na michezo (karate, judo na baseball) nk.

Kuhusu WATATU Ltd.

Kampuni iliundwa na Wajapani watatu wa kujitolea, Ryuta Okamoto, Yuki Mito, Sho Izaki, na jina la kampuni hiyo linatokana na neno la Kiswahili la watatu ikimaanisha kuwa Kampuni hiyo ilianzishwa na hao watu watatu.

Bwana Ryuta OKAMOTO, Afisa Mtendaji Mkuu wa WATATU, alifanya kazi ya kujitolea kama Afisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Ruvuma. Bwana Yuki MITO, Mkurugenzi wa WATATU, alifanya kazi ya kujitolea kama Afisa Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Morogoro na Bw. Sho IZAKI, Mkurugenzi wa WATATU, alifanya kazi ya kujitolea kama Mwalimu wa Mazoezi ya Viungo, Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Songea huko Ruvuma.

PhotoMkuu wa WATATU anatoa ushauri kwa wakulima

PhotoMkulima wa Mpunga anafurahia kilimo


Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
JICA Tanzania Office, P.O. Box 9450,
Dar es Salaam, Tel: 022-211327/30
Ms. Noriko Ogasa: Ogasa.Noriko@jica.go.jp
Ms. Catherine Shirima: ShirimaCatherine.Tz@jica.go.jp

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency