Japan International Cooperation Agency
Share
  • 日本語
  • English
  • Français
  • Espanol
  • Home
  • About JICA
  • News & Features
  • Countries & Regions
  • Our Work
  • Publications
  • Investor Relations

Taarifa kwa Umma

07 Oktoba 2022

JATA Yachukua Hatua Kupunguza Uhalifu kwa Vijana Zanzibar

Jumuiya ya Wahitimu wa JICA Tanzania (JATA) imefanya semina katika Taasisi ya Elimu kwa Wahalifu (the Institution of Education for the offenders) huko Kilimani, Zanzibar kusambaza ujuzi wao walioupatikana kupitia programu za mafunzo ya JICA (KCCP) ili kupunguza idadi ya kesi za uhalifu kwa vijana Kisiwani humo.

Ajenda kuu ya "Upatikanaji wa Haki", inaakisi ongezeko kubwa la uhalifu ya kijamii miongoni mwa vijana visiwani Zanzibar, na kusababisha matukio ya kutisha na kuongeza kasi ya vijana kuhukumiwa vifungo katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Warsha hiyo iliangazia makuzi ya vijana hadi kufikia utu uzima kwa kubainisha mambo yanayopelekea vijana kujiingiza kwenye uhalifu na kutoa mbinu mbadala hususani fursa zilizopo katika fani za uvumbuzi na ujasiriamali ili kuepukana na uhalifu.

Mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Zanzibar Magharibi Mh. Idrisa Kitwana Mustafa, Kamishna wa Taasisi ya elimu Bwana Hamis Bakari Hamis, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Zanzibar Dk. Idrisa Muslim, Mkurugenzi wa Maji na Nishati Zanzibar Bwana. Mudrik Abbas na Waziri wa Ujenzi mstaafu wa Zanzibar Dk. Sira Mamboya. Wanachama wa JATA wapatao 45, Wafungwa wawili waliomaliza adhabu, wahitimu wawili wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu kwa Wahalifu pia walihudhulia.

Mh. Kitwana aliipenda kaulimbiu kwa kuwa inaendana na sera ya serikali ambayo imekuwa ikisaidia kukabiliana na tatizo la ongezeko la idadi ya vijana katika Taasisi ya Elimu kwa Wahalifu Zanzibar na nchi nzima.

Alisisitiza juu ya uanzishwaji wa sera ya Vijana na kutambua vipaji kwa vijana kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi na kupunguza vitendo vya uhalifu. Aliwataka vijana kutumia vipaji vyao kufanya mabadiliko chanya katika maeneo yao ya kazi.

Gregory Mlay, Mwenyekiti wa JATA alikiri kwamba JICA imekuwa mstari wa mbele kushiriki katika maendeleo ya nchi na imekuwa ikisaidia mafunzo mbalimbali kwa Watanzania.

Aliongeza kuwa JATA imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali kila mwaka ili kuendelea kuimarisha ushirikiano wake na Japan pamoja na kuwasaidia watanzania wanaoungwa mkono na JICA.

"Tukio hili ni fursa ya kutumia ujuzi na maarifa tuliyopata huko Japani kwa manufaa ya jamii, maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla," alibainisha.

Katika hatua nyingine wanachama wa JATA walijadili njia kadhaa za kuwaelimisha vijana na kuwasaidia katika kukuza ujuzi kupitia mafunzo na ushauri ili kutengeneza fursa za ajira zinazofaa kwa kizazi cha sasa na kijacho. Mjadala huo ulikuwa na dondoo za kupunguza kasi ya vifungo kwa vijana pamoja na kuleta uelewa kwa jamii kuacha kuwabagua wafungwa wanaomaliza vifungo na kutoka gerezani.

PhotoPresentation on Youth's Criminology in Zanzibar during the workshop at the Institution of Education for the offenders, Kilimani - Zanzibar

PhotoThe Institution of Education for the offenders' Farm visit located at Hanyegwa Mchana


For more information about press conference, please contact:
Ms. Aoki Yu: Aoki.Yu@jica.go.jp
Ms. Evona Mathew: Mathew-Evona@jica.go.jp
JICA Tanzania Office
P.O. Box 9450, Dar es salaam
Tel: +255-22-2113727/30

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency