Japan International Cooperation Agency
Share
  • 日本語
  • English
  • Français
  • Espanol
  • Home
  • About JICA
  • News & Features
  • Countries & Regions
  • Our Work
  • Publications
  • Investor Relations

Taarifa kwa Umma

16 Mei 2023

MRADI WA JICA KUHAMASISHA MATUMIZI YA GESI ASILIA TANZANIA

Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani (JICA) na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati zimesaini Mkataba wa Majadiliano (Record of Discussion R/D) kwa ajili ya ushirikiano wa kiufundi katika matumizi bora ya gesi asilia.

Tarehe 16 Mei 2023, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi . Felchesmi Mramba na Mwakilishi Mkuu wa JICA Bw. ARA Hitoshi walisaini mkataba huo kama makubaliano ya kutekeleza Mradi huo uliopewa jina la "Mradi wa Kuendeleza Uwezo wa Matumizi ya Gesi Asilia Tanzania".

JICA imekuwa ikisaidia maendeleo ya serikali ya Tanzania kwa zaidi ya miaka 60 tangu miaka ya 1960 kwa kuzingatia mtazamo wake wa "Kuongoza dunia kwa uaminifu". Ushirikiano katika sekta ya nishati nchini Tanzania umedumu kwa zaidi ya miaka 40.

Kabla ya kusaini makubaliano hayo JICA ilituma Wataalamu kuja Tanzania kufanya utafiti wa mipango huo kwa kina kuanzia tarehe 23 Februari hadi 12 Machi, 2023 ili kuandaa Mradi huo. Wataalamu hao walifanya majadiliano na Wizara ya Nishati, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na wadau wengine ili kuandaa mpango wa kina wa mradi huo.

Mradi huo umelenga kukuza matumizi bora ya gesi asilia nchini Tanzania kwa ajili ya ukuaji wa uchumi kwa njia rafiki kwa mazingira. Mradi huo pia unalenga kuimarisha uwezo wa kupanga na kutekeleza matumizi ya gesi asilia nchini.

Muda wa mradi unakadiriwakuwa miezi 24, kuanzia Oktoba 2023 hadi Septemba 2025.

Mradi huo utakuza matumizi ya gesi asilia nchini Tanzania kwa uwiano na ukuaji wa uchumi na masuala ya mazingira kwa kuhuisha Mpango wa Taifa wa Matumizi ya Gesi (NGUMP), kuandaa mfumo wa kisheria unaohitajika kwa matumizi ya gesi na kujenga uwezo wa watumishi wa Wizara ya Nishati, TPDC na EWURA ili kutekeleza na kudhibiti matumizi ya gesi asilia na kuchangia maendeleo na ukuaji wa uchumi wa nchi.

Mwisho.

PAGE TOP

Copyright © Japan International Cooperation Agency